Moja ya Mabweni Ya Wanafunzi Wa Kitivo Cha Kompyuta UDOM(Picha kutoka Maktaba)
Kitivo Cha Maswala Ya Kompyuta Katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Kilifungwa Takribani Miezi Miwili iliyopita Baada ya Wanafunzi wa kitivo hiko kuandamana kwa siku tatu mfululizo na kupelekea chuo hiko kufungwa kwa sababu ya wanafunzi hao kuandamana kwaajili ya kudai pesa zao za kitivo maalumu.
Katika harakati za kudai pesa za kitivo maalumu wanafunzi takribani 27 waliweza kusimamishwa masomo mara baada ya kuonekana kuwa wao ndio vinara wa mgomo huo.Kitu kilichopelekea wanafunzi wenzao kuendelea kugoma ili kushinikiza uongozi wa chuo kuwarudisha wenzao ambao walisimamishwa masomo.
Wakati wanafunzi wakiwa katika mgomo ili kushinikiza uongozi wa chuo uwarudishe wanafunzi wenzao Uongozi Wa Chuo Uligoma Kuwarudisha wanafunzi hao 27 na hatimaye kufunga kitivo kizima kilichopelekea wanafunzi hao kupewa masaa 10 kuondoka katika eneo la chuo.
Uongozi Wa Kitivo Hiko Umeamua Kuwarudisha Wanafunzi Hao Kwa masharti ya wanafunzi kuwataja nani na nani walikuwepo kwenye maandamano hayo na mgomo uliotokea katika kitivo hiko.
Vuta Subira Tutazidi kuwajuza.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)