WASHIRIKI WA MISS DAR CITY CENTER WAJIFUA KWA AJILI YA SHINDANO LA MEI 13 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASHIRIKI WA MISS DAR CITY CENTER WAJIFUA KWA AJILI YA SHINDANO LA MEI 13


Hawa ndiyo warembo 18, wanaotarajia kushiriki katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Dar City Center 2011, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazoezi yao ya kujiandaa na shindano hilo linalotarajia kufanyika Mei 13 mwaka huu katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada Ilala Dar es Salaam.

 

Jumla ya Warembo 18, wameanza mazoezi ya pamoja katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada Ilala Dar es Salaam jana kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka Miss Dar City Center 2011, linalotaraji kufanyika kwenye Ukumbi huo huo Tarehe 13 mwezi wa tano mwaka huu. Warembo hao wakiwa katika mazoezi ya kudansi.
Mazoezi ya kutembea 'Cat Walk'...
Hizi ni baadhi ya Pozi za picha kutafuta nani mkali anaweza kuibuka katika Kategoli ya 'Photo Genic'
Si doli la dukani bali ni pozi la picha....
Si kwamba anaogopa kamera la hasha, bali ni pozi tofauti la kivyake, inaelekea utotoni aliupenda sana mchezo wa kujificha!..
Baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika mashindano hayo yaliyopita wakiwa ukumbini humo kuangalia mazoezi hayo. 
Na Sufiani Mafoto

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages