VODACOM YAKABIDHI PESA KWA WASHINDI WAO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VODACOM YAKABIDHI PESA KWA WASHINDI WAO

 Innocent Joseph fundi seremala wa Mbezi Juu jijini akiwa ameshikilia hundi yake ya shilingi milioni kumi aliyokabidhiwa na Vodacom Tanzania baada ya kushiriki katika promosheni ya siku ya uwezo iliyoendeshwa na kampuni hiyo.
Mshindi wa promosheni ya siku ya uwezo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Yuda Joseph mfanyakazi wa dukani eneo la Kinondoni jijini akiwa ameshikilia hundi ya shilingi milioni kumi aliyokabidhiwa na Vodacom Tanzania baada ya kushiriki na kushinda kupitia promosheni hiyo.
 Mshindi wa promosheni ya siku ya uwezo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Yuda Joseph mfanyakazi wa dukani eneo la Kinondoni jijini akimuhudumia mteja mara baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi aliyojishindia kupitia promosheni hiyo.
 Meneja Udhamini na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akifafanua jambo kwa wanafunzi wa Chuo Kishiriki cha Ualimu Chang’ombe DUCE jinsi mwanafunzi mwenzao Gaspary  Kasmiry aliyeshikilia hundi alivyoshiriki na kushindia kitita cha shilindi milioni kumi katika promosheni ya siku ya uwezo iliyoendeshwa na kampuni hiyo.
Meneja Udhamini na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa, Mshindi wa promosheni ya siku ya uwezo inayoendeshwa na kampuni hiyo, Fadhil Felix, Mwanahabari Kambi Mbwana na Mtaala wa Masuala ya Habari  Matina Nkurlu wakiteta jambo mara baada ya kumkabidhi Felix hundi ya shilingi milioni kumi aliyojishindia kupitia hiyo.
--
Na Mwandishi Wetu. 
Washindi saba kati ya 10 waliojishindia vitita vya shilingi milioni 10 kila mmoja katika promosheni ya ‘Siku ya uwezo’iliyochezeshwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania, mwishoni mwa wiki wamekabidhiwa hundi zao, baada ya kushinda shindano hilo. 
Shindano hilo lilichezeshwa Aprili 4 mwaka huu, huku likiwataka wateja wao watume ujumbe mfupi wa maneno kuzungumzia malengo yao, endapo watafanikiwa kushinda Sh Milioni 10. 

Timu ya watendaji wa Vodacom Tanzania ikiongozwa na Meneja Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo, Rukia Mtingwa, ilitembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ili kujionea mazingira wanayoishi wateja hao walioshinda fedha hizo. 
Akizungumza na waandishi wa Habari, Rukia alisema kwamba ziara hiyo ya siku nzima, ililenga kujua mazingira wanayoishi wateja wao wote ikiwemo wale wa mikoani mara baada ya washindi hao kuingiziwa fedha zao kwenye akaunti zao za benki. 
Alisema shindano la Siku ya Uwezo lilibuniwa ili kuleta changamoto na kutimiza malengo kwa wateja walioamua kujitolea na kushikiriki promosheni hiyo. 

“Nimefurahi kuona mazingira tofauti ya wateja wetu ambao ni washindi wenye bahati ya Siku ya Uwezo ya Vodacom. Ni matarajio yangu washindi wetu watazitumia pesa hizi vizuri kama walivyoandika meseji zao, wakiainisha  malengo yao endapo watafanikiwa kushinda,” alisema Mtingwa. 

Washindi hao wenye bahati ni pamoja na Innocent Julius Tete (Mbezi Juu), Yuda Joseph Mang’anya (Kinondoni), Gaspary Kasimiry Kamina (Chang’ombe), Fadhiri Felix Gwabisaba (Yombo Kilakala), Kombo Ally Athuman (Kipunguni B Ukonga), Judith Peter Ruge (Mongolandege) na Ibrahimu Abdallah Msigwa (Mbagala). 

Kampuni ya Simu ya Mikononi ya Vodacom Tanzania, imekuwa ikichezesha promosheni mbalimbali kwa nia ya kuwawezesha wateja wao. Kupitia promosheni hii ya Siku ya Uwezo Zaidi, jumla ya wateja 10, waliibuka na ushindi huo. Kati ya hao miongoni mwao saba walitokea jijini Dar es Salaam wakati wengini ni wa mikoa ya Mwanza na Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages