TLS: MUSWADA WA KATIBA MPYA UNA KASORO, TUNNAPANGA KUMUONA RAISI KIKWETE KUMSHAURI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TLS: MUSWADA WA KATIBA MPYA UNA KASORO, TUNNAPANGA KUMUONA RAISI KIKWETE KUMSHAURI

 Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Francis Tola,akitoa tamko la chama hicho kuhusu muswada wa sheria ya Katiba mpya, alipozungumza na waandishi wa habari, jana kwenye Ofisi za TLS, mjini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu wa Rais wa TLS Mpale Mpoki na Mtendaji Mkuu wa TLS,  Emilia Siwingwa.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Rais wa Chama hicho, amesema, kwa ujumbla muswada ni mzuri kutokana na maudhui yake, lakini una kasoro nyingi ambazo ikiwemo kuwanyima wananchi wengi kushiriki katika kutoa maoni.

Alisema, hatua ya muswada huo kupelekwa bungeni kwa hati ya dharura, kunasababisha muswada huo kujadiliwa na makundi machache ya wananchi kama ambavyo sasa maoni yanafanyika Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar badala ya kuwa nchi nzima.
Rais Tola amesema, kutokana na kasoro ambazo TLS imebaini itakwenda kwa Rais Jakaya Kikwete kujaribu kumshauri mambo kadhaa na mapendekezo yao ikiwemo kuondoa hati ya dharura.Picha na Habari na Mdau Bashir Nkromo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages