TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA MIAKA 23 YAAGWA LEO KUELEKEA UGANDA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA MIAKA 23 YAAGWA LEO KUELEKEA UGANDA



Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Kanali Mstaafu, Iddi Kipingu akiwapiga msasa wachezaji wa timu hiyo. Kushoto ni Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
 
Kapteni Wa Timu Hiyo Shabani Kado Akiongea na Kuahidi Ushindi
 
Kocha Jamhuri Kiwelo aka Julio Akiteta Mbele ya Raisi Wa TFF Leordiga Chilla Tenga Na Mh Idd Kipingu

 
Wachezaji Wa Timu Hiyo Waliondoka Leo kuelekea Uganda


Mwenyekiti Wa Baraza La Michezo (BMT) Kanali Mstaafu Iddi Kipingu Akimkabidhi Bendera Ya Taifa Kapteni Wa Timu Shabani Kado Kabla Ya Timu Hiyo Kuondoka Kuelekea Uganda
.............
Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 imeagwa leo mchana katika ofisi za TFF kabla ya uondoka  baadaye kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya mchujo ya michezo yaAfrika (All Africa Games) itakayochezwa Jumamosi  hii.
       Msafara wa timu hiyo utakuwa na jumla ya watu 29, wakiwemo wachezaji 21 na benchi la ufundi lenye watu sitaukiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar(ZFA), Hafidh Ally Tahir.
       Wachezaji watakaokuwemo katika msafara huo niShaaban Kado, Juma Abdul, David Luhende, Babu Ally, Shomari Kapombe, Jabir Aziz, Salum Aboubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Kigi Makasi, Gharib Mussa, Mbwana Bakari, Idrisa
Abdulrahim, Innocent Wambura, Khamis Mcha, Awadh Issa, Amour Suleiman, Himid Mao, Mrisho Ngassa na Salum Telela. 
    Aprili 13 mwaka huu timu hiyo ilikabidhiwa jumla ya sh. milioni2 2 ambazo iliahidiwa endapo ingeitoa Cameroon kwenye michuano ya Olimpiki. Fedha hizo ziliahidiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya
Simba Trailers. 
      NSSF kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake Dk. Ramadhan Dau ilikabidhi sh. milioni 10, wakati Azim Dewji ambaye ni Mkurugenzi wa Simba Trailers alikabidhi sh. milioni 12.
      Kati ya fedha hizo ilizotoa Simba Trailers, sh. milioni 10 ni kwa ajili ya timu, sh. milioni 2 kwa ajili ya kipa aliyeokoa penalti na wafungaji wa
mabao mawili ya U23. 
     U23 imepangiwa kucheza na Nigeria katika raundi ya pili ya michuano ya Olimpiki ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Juni 4 na 5 mwaka. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages