TIGO YATATUA TATIZO LA MAJI KWA WANAWAKE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TIGO YATATUA TATIZO LA MAJI KWA WANAWAKE

Wanamuziki kutoka kundi la Wanaume Famili Chege na Temba wakifanya makamuzi ya kufa mtu katika hafla hiyo.
Mwanamuziki kutoka nyumba ya kukuza vipaji THT, Mwasiti Almasi (katikati), akifanya  makamuzi ya nguvu na wanenguaji wake.
Mwasiti (mbele), akiimba wimbo wa ‘Hao’ na kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ilack Jackson, baada ya kumchagua aimbe kama Chidy Benzi.
Balozi wa maji, Jokate Mwegelo, akiongea jambo kwenye hafla hiyo.
KAMPUNI ya masiliano ya simu za mkononi Tanzania ya Tigo, mapema leo imeitisha matembezi ya hiari kwa ajili ya kuchangisha fedha za kujengea visima katika Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani, 

Matembezi hayo yenye lengo la kuonyesha umuhimu wa maji hasa kwa wanawake ambao hutembea kwa muda mrefu na ndoo za maji kichwani, yalianzia eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam, na kuzunguruka kupitia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Ubungo na kumalizikia katika viwanja vya Mlimani City  ambako kulikuwa na shoo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

Akiongoe katika hafla hiyo, Balozi wa maji,  Jokate Mwegelo, alisema  kuwa anafurahi sana kampuni ya Tigo kuguswa na tatizo hilo la uhaba wa maji nchini, akasema:

“Nimefurahishwa sana na Tigo kwa kuliona tatizo la maji nchini na kuamua kuitisha uchangiaji wa pesa kwa ajili ya kujenga visima kwa kila mwaka kama walivyosema tena wakiaanza na Bagamoyo”, alisema Jokate.nzi.

Picha/Stori: Musa Mateja/GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages