Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige (wa pili kulia) wakati akizindua mashindano ya mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni Wilayani Karatu juzi. Wengine kushoto ni Asaf Simantov wa TIGO, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mathew Sondoweko na Zainab Ansell wa Zara Tours mwenye nguo nyekundu. Kulia kabisa ni Mkuu wa Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro Benard Mrunya. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Mwanariadha Ally Athumani akishiriki katika mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni zilizofanyika juzi Wilayani Karatu chini ya udhamini wa Kampuni ya Simu za mkononi ya TIGO. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Washiriki katika mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni wakijiandaa kuanza mbio juzi Wilayani Karatu. Katika mbio hizo Mary Naali aliibuka mshindi kwa wanawake wakati Fabian Joseph alikuwa mshindi wa kwanza kwa wanaume. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)