Baadhi ya vijana waliofika kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuchangia mawazo yao kuhusu Mjadala wa Katiba mpya, wakiwa nje ya ukumbi huo baada ya kufika ukumbini hapo na kukuta ukumbi huo ukiwa umefurika watu na kukosa nafasi. Imeelezwa na vijana hao kuwa ukumbini humo waliruhusiwa hadi watoto wasiokuwa na uwezo wa kuchangia jambo ambalo lilisababisha kujaa kwa ukumbi huo na kuwanyima fulsa ya kuchangia watu wenye uwezo wa kufanya hivyo. "ili kuepuka yasitokee kama yaliyowakuta wenzetu wa Dodoma jana ndiyo maana tumeamua kukaa tu hapa nje" alisema mmoja wa vijana hao. Mmoja kati ya vijana waliofanikiwa kuwahi na kuingia ukumbini humo, akichangia mjadala huo.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)