MCHAKATO WA KUJADILI MUSWADA WA KATIBA MPYA WAINGIA DOA BAADA YA MABOMU YA MACHOZI KURINDIMA MKOANI DODOMA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MCHAKATO WA KUJADILI MUSWADA WA KATIBA MPYA WAINGIA DOA BAADA YA MABOMU YA MACHOZI KURINDIMA MKOANI DODOMA LEO

 Baadhi ya wadau wakitoa maoni yao ndani ya Ukumbi wa Pius Msekwa leo mjini Dodoma.
 Wananchi,viongozi mbalimbali, wabunge na wadau kutoka asasi mbalimbali wakifuatilia masuala mbalimbali kuhusu mchakato wa utaratibu wa kuandika katiba mpya ya nchi ndani ya ukumbi wa Pius Msekwa  leo mjini Dodoma.
 Wakazi wa Dodoma wakiwa wamejitokeza  nje ya ukumbi wa bunge kutoa maoni yao juu ya mchakato wa kuanzishwa kwa mchakato wa utaratibu wa kuandika katiba mpya leo mjini Dodoma na kulazimisha kufungwa kwa  muda barabara kuu ya Dodoma – Dar es salaam inayopakana na ukumbi huo.
 Pichani Juu na Chini Nje ya eneo la geti la ukumbi wa bunge wananchi wakisubiri kuingia ndani ya ukumbi wa Pius Msekwa ambako ndiko shughuli  za ukusanyaji wa maoni ya mchakato wa kuanzisha utaratibu wa kuandika katiba mpya ulikuwa ulikuwa ukiendelea leo mjini Dodoma.
 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi katika eneo la ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma
 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwatawanya wananchi  kwa kuwafyatulia mabomu ya machozi (wengi wao wakiwa wanafunzi wa vyuo  mjini Dodoma) waliozusha vurugu  ya kutaka kuingia ndani ya eneo la  bunge  kutoa maoni yao.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma  Dkt. James Msekela akiongea na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi  wa vurugu zilizotokea nje ya geti la ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages