MAONYESHO YA HARUSI YAANZA LEO DIAMOND JUBILEE YAKIWA NA WASHIRIKI ZAIDI YA 50. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAONYESHO YA HARUSI YAANZA LEO DIAMOND JUBILEE YAKIWA NA WASHIRIKI ZAIDI YA 50.

 Mmoja wa waliotembelea maonyesho ya HARUSI kwenye ukumbi wa DIAMOND JUBILEE wakisiliza maelezo toka kwa washiriki wa maonyesho hayo
Wfanyakazi wa Blue Pearl Hotel & Apartment wakijiweka sawa kwa maonyesho ya HARUSI ndani ya Diamond.
Kumbu kumbu ni muhimu katika matukio kama ya HARUSI, GRM Production, wataalam wa picha wakiwa ndani ya maonyesho ya HARUSI Diamond Jubilee
--
Maonyesho ya Harusi yaliosubiriwa kwa hamu na wadau mbalimbali wa masuala ya harusi na watarajiwa wa harusi yameanza leo katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE huku yakiwa na washiriki zaidi ya 51 waliochukua mabanda kwa kuonyesha na kuuza biashara zao.

Wakizungumza kkwa nyakati tofauti tofauti washiriki hao ambao wamejitokeza kwa wingi, waliyasifu maonyesho ya mwaka huu na kusema kuwa yamekuwa hai na mvuto wa aina yake, kwa kuwa mambo mengi yameongezeka kwa mwaka huu.

"tulishiriki mwaka jana, na mwaka huu pia, ila mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi na yenye kupangiliwa zaidi, kwa kweli waandaaji wamejipanga vilivyo" alisema mmoja wa washiriki toka kampuni ya picha ya GRM.

Maonyesho ya mwaka huu yameongezewa ladha kwa kuongezewa vitu mbaliombali, ambapo mbali na kuongezeka kwa nafasi na mabanda, pia kuna upya wa vitu  kama 'mdahalo wa Harusi' ambapo wataalamu waliobobea katika masuala ya harusi watazungumza na wale watakaotembelea maonyesho hayo.

Huku jarida la kwanza na la aina yake la kitanzania 'HARUSI MAGAZINE' chini ya usimamizi wa mbunifu wa mavazi maarufu nchini Mustafa Hassanali likisambazwa ukumbini hapo kwa toleo lake la kwanza.
Wadau wote na wakaazi wa jiji la Dar ess salaam wanakaribishwa sana katika maonyesho haya ya siku tatu yanayoendelea ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mfaume Shaban
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali

PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania

105 Kilimani Road,   Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania

(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)

Tel :  +255 (0)22 266 8555
Mobile :  +255 (0)655 501 526

Mail : media@mustafahassanali.net

Web : www.mustafahassanali.net

www.swahilifashionweek.com

www.harusitradefair.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages