MAMA SALMA KIKWETE ATUA MKOANI LINDI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAMA SALMA KIKWETE ATUA MKOANI LINDI

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akipokewa na viongozi  mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani  Lindi Jana. Mama Salma Kikwete yuko mkoani  humo kushiriki na kuhimiza shughuli za maendeleo ya  wananchi.Picha na Aron Msigwa-MAELEZO
---
Na.Anna Nkinda – Maelezo, Lindi.
Wenyeji wa mikoa ya Lindi na Mtwara wametakiwa kutouza ardhi yao kiholela kwa wageni  badala yake waitumie ardhi hiyo kwa kilimo na shughuli zingine za maendeleo.
Wito huo umetolewa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati akiongea na viongozi pamoja na watendaji wa mikoa hiyo.

Mama Kikwete alisema kuwa mikoa hiyo imejaliwa kuwa na ardhi nzuri na yenye rutuba jambo ambalo linawafanya wageni  wengi kukimbilia  katika mikoa hiyo kwa nia ya kutaka kununua ardhi.

“Katika maeneo mengine watu wanagombania ardhi na kupata kipande kidogo cha ardhi ni kazi kubwa lakini ninyi mmejaliwa kuwa na ardhi nzuri, kubwa na yenye rutuba hivyo basi muitumie ardhi hii kuzalisha chakula”, alisema Mama Kikwete.

Aliendelea kusema kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara imejaliwa kuwa na Gesi  ya asili jambo ambalo si la kawaida katika maeneo mengine  hivyo basi kama watauza ardhi wajue kuwa wageni watakuja na kunufaika na gesi hiyo kuliko wenyeji wa eneo husika.

Pia amewataka viongozi hao kabla ya kusaini mikataba au kuingia katika makubaliano yoyote yale wasome kwa umakini mkubwa nyaraka wanazopewa ili mikataba hiyo isije ikaleta matatizo  siku za usoni.

Kwa upande wa madiwani alisema kuwa madiwani wananguvu sana katika maeneo yao ya kazi kwani bila Diwani kusema mambo hayaendi. Alitoa mfano kama kuna mradi wa kuchimba kisima wao madiwani wajiulize je thamani ya kisima ni sahihi?

Alimalizia kwa kuwasihi madiwani hao kutokubali kukosa vikao vya kazi  labda wawe wagonjwa kwani kuwepo kwao katika vikao hivyo kuna umuhimu mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages