MAJAMBAZI YAPATA KIPIGO KITAKATIFU KUTOKA KWA ASKARI WA JESHI LA POLISI JIJINI MWANZA JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAJAMBAZI YAPATA KIPIGO KITAKATIFU KUTOKA KWA ASKARI WA JESHI LA POLISI JIJINI MWANZA JANA


Jana majira ya saa kumi na dakika kadhaa jioni jeshi la polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwatia nguvuni watu wanne wanaotuhumiwa kwa kufanya ujambazi wakiwa na bunduki moja aina ya smg na bastola mbili moja ikiwa na risasi 12 na na ya pili ikiwa na risasi 2.
 
Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la polisi Mwanza Simon Sirro amesema kuwa watu hao wamekematwa katika eneo la mtaa wa libert jirani na benki ya NMB wakiwa kwenye harakati za safari kuelekea Nyegezi ambako walipanga kwenda kufanya uvamizi kwenye duka moja.
Awali majambazi hayo yalivamia bar moja eneo la kilimahewa na kuwalaza watu chini kisha kupora mali zao na kuiba bastola ya mteja mmoja. Majambazi hayo yaliyokuwa katika gari dogo yalipostukia kuwa yanafuatiliwa yalianza kufyatua risasi hovyo hali iliyosababisha shughuli za biashara kwenye eneo la tukio kusimama kwa muda.
Raia wema ndiyo waliofanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambao nao bila ajizi walifuatilia nyendo za majambazi hao na hatimaye kufanikiwa kuwatia nguvuni.
Wawili kati ya majambazi hayo manne hali zao ni mbaya na wamepelekwa hospitali ya Rufaa Bugando, mmoja katwangwa risasi mguuni na takoni ile hali mwingine sugu anayetambulika kwa jina maarufu 'Askofu' akiwa amevunjika mguu kabisa kwa kutwangwa risasi wakati alipojaribu kuitoroka mikono ya polisi.
"Watu wanatafuta fedha kwa njia zisizo halali kwa kutumia nguvu na hata kufanya mauaji ili wapate fedha kwaajili ya sikuu ya pasaka, napenda kuwatahadhalisha wote waliopanga kuingia Mwanza kufanya uhalifu kuwa waondoke wakiwa wameaga makwao kwani hawatatoka wakiwa salama" amesema kamanda Sirro.
Jeshi la polisi mwanza linaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio zima sambamba na kuwahoji watuhumiwa wote wanne wa mkasa huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages