JULIO AWAITA NGASSA, KIGI MAKASSY KUIVAA CAMEROON - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JULIO AWAITA NGASSA, KIGI MAKASSY KUIVAA CAMEROON

 
Na Khadija Mngwai
KIUNGO mshambuliaji Mrisho Ngassa, Kiggi Makassy na Jabir Aziz ni miongoni mwa wachezaji saba waliochaguliwa kuongeza nguvu katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 (U23), Manyara Stars kitakachoivaa Cameroon Aprili 9, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Manyara Stars iliyo chini ya Kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ (pichani), inahitaji ushindi wa bao 1-0 au tofauti ya mabao mawili katika aina yoyote ya ushindi itakayopata ili iweze kusonga mbele katika michuano ya kufuzu kushiriki michezo ya Olimpiki mwakani huko England. Katika mchezo wa awali huko Younde, Cameroon, Manyara ililala 2-1.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema, wachezaji hao wameongezwa katika kikosi hicho ili kuhakikisha Manyara Stars inasonga mbele.

“Benchi la ufundi lilifanya kazi na kuona wachezaji hao wanafaa kuwamo katika kikosi hicho ili kuisaidia timu kuweza kuifunga Cameroon na kusonga mbele, tunaamini wachezaji hawa watawajibika ipasavyo katika majukumu waliyopewa,” alisema Wambura.

Mbali ya Kiggi (Yanga) na Ngassa na Jabir wa Azam kuitwa katika kikosi hicho, wengine walichaguliwa kujiunga na Manyara ni Juma Abdul na Ally Lundenga wa Mtibwa Sugar, David Luhende na Kelvin Charle wa Simba.

Wachezaji hao wanajiunga mara moja na kambi ya timu hiyo iliyopo Bamba Beach Kigamboni, Dar es Salaam chini ya Julio.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages