Mchungaji Mstaafu Mwaisapile akipokea zawadi ya simu ya Mkononi kutoka airtel. anayemkabidhi ni meneja wa biashara wa Airtel Mkoa wa Arusha, Paschal Bikomagu. Kulia DC, ngorongoro.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Bw Elias Wawa Lali (katikati), Diwani wa Kata ya Samunge, Bw Jackson Sandea (kulia), Meneja Biashara wa Airtel mkoa wa Arusha, Paschal Bikomagu-
Ikiwa ni muendelezo wa kutimiza ahadi yake ya kuleta mawasiliano nafuu na yenye kuwafikia watanzania wengi zaidi, hasa walioko maeneo ya vijijini hapa nchini, kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel, leo imetangaza kuzidi kupanua mtandao wake kwa kuzindiua huduma ya mawasiliano katika eneo la Samunge na maeneo jirani, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.Kwa mujibu wa Airtel Tanzania, kuzinduliwa kwa mtandao imara na wenye nguvu umegharimu zaidi ya dola za kimarekani laki moja na nusu hadi ulipomalizika. Uwekezaji huu utawezesha kuleta mawasiliano thabiti kwa watu wa vijiji vya Samunge, Mgongo, Mageri, Yasimdito and Digodigo.
Akitoa maoni yake juu ya uzinduzi huu wa huduma ya mawasiliano, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sam Elangalloor amesema kwamba Airtel imejidhatiti vilivyo katika kutoa huduma bora na nafuu kwa watu wa Samunge, huduma inayoambatana na uwepo wa mtandao madhubuti pamoja na huduma nyingine lukuki ambazo zimekuwa zikipatikana na kufurahiwa na wateja wengine wa Airtel Tanzania nzima.
“Uwepo wetu wetu Samunge na maeneo mengine ya jirani, kwa hakika kutaleta chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi na wageni wa maeneo haya. Kuwaunganisha watu wa Loliondo wakati huu ambapo mahitaji ya mawasiliano ni makubwa, kunadhihirisha dhamira yetu ya kuwa mbele zaidi kwa kila tunalofanya”, alieleza zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)