MBUNGE wa jimbo la Ilala(CCM) Musa Azzan ‘Zungu’
--
MBUNGE wa jimbo la Ilala(CCM) Musa Azzan ‘Zungu’ amewasilisha pingamizi la awali katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi la aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo katika Uchuguzi Mkuu wa mwaka 2010,Hamad Tao linalotaka mahakama hiyo imsamehe kulipa dhamana ya kesi hiyo.
Katika kesi hii ya Uchaguzi Na.104/2010, Tao ambaye hana wakili anamshtaki mbunge wa Jimbo hilo Mussa Azzan anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Tadayo, aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wanatetewa na wakili wa serikali Rashid Karimu.Katika kesi ya msingi Tao anaimba mahakama itengue ubunge wa Zungu kwasababu hakushinda kihalali na taratibu za sheria ya Uchaguzi zilikiukwa.
Kesi hiyo ambayo ilikuja jana kwaajili ya kutajwa mbele ya Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi wakili wa mdaiwa Zungu(Tadayo) aliambia mahakama amewasilisha pingamizi dhidi ya mlalamikaji(Tao) la kutaka mahakama ikatae ombi la mlalamikaji lakutaka mahakama hiyo itoe amri ya kumsamehe asilipe dhamana ya kesi hiyo ambayo ni sh milioni tano kwa kila mdaiwa. Kwa Habari zaidi bofya na Endelea......>>>>>>

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)