WASANII WA KIKUNDI CHA SURVIVAL SISTERS WAKABIDHIWA BAJAJI IKULU LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASANII WA KIKUNDI CHA SURVIVAL SISTERS WAKABIDHIWA BAJAJI IKULU LEO

Kaimu Mnikulu Mkuu Kassimu Mtawa (katikati) akikabidhi Bajaji mbili zenye thamani ya Sh. milioni 9.5 kwa wasanii wa Kikundi cha Muziki cha Survival Sisters zilizotolewa. Bajaji hizo zilikabidhiwa na Mnikulu Mkuu kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni utekelezaji wa ombi la wasanii hao waliomtumia. Kushoto ni Irine Malekela na kulia ni Ratifa Abdallah. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
Mmoja wa wasanii wa Kikundi cha Survival sisters, Irine Malekela, akijaribu kuendesha pikipiki ya matairi matatu maarufu kama Bajaji walizokabidhiwa na Kaimu Mnikulu Mkuu Kassim Mtawa, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni sehemu ya Rais Kikwete kutekeleza ombi la kikundi hicho la kuwasaidia usafiri utakaowawezesha kuendeleza vipaji vyao vya muziki. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
Ratifa Abdallah, akijaribu kuendesha pikipiki ya matairi matatu (Bajaji) baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mnikulu Mkuu Kassim Mtawa, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ombi la kikundi hicho kwa Rais kuwasaidia usafiri utakaowawezesha kuendeleza vipaji vyao vya muziki.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages