Mbunge wa Urambo Mashariki Samwel Sitta
---
UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umeanza kutekeleza kwa vitendo azimio lake la kuahidi kupambana na viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kutoa matamko bila kufuata utaratibu, kwa kutangaza kumvua nafasi ya ulezi wa UVCCM Mkoa wa Tabora, Spika wa zamani, Samuel Sitta.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Baraza Kuu la UVCCM, lilitangaza baada ya kikao chake Dodoma, kuwa katika kukabiliana na viongozi hao, litahakikisha viongozi wa CCM wanaotoa matamko bila kufuata utaratibu, hawapati nafasi yoyote ya uongozi na chama kisiwateue kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi ujao.
Walikitaka chama hicho kuwaelekeza viongozi wake, umuhimu wa kuzingatia maadili na nidhamu kwa kutumia vikao kuwasilisha hoja zao, na si kutumia matamko kukidhoofisha na kujijengea umaarufu binafsi.
Kutokana na utekelezaji wa azimio hilo, jana Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga, alitangaza kuwa wamemvua Sitta ulezi wa UVCCM Mkoa kutokana na kuendelea kutoa kauli licha ya azimio hilo. Sitta ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki mkoani humo, anadaiwa kuponzwa na kauli aliyoitoa na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, akisema UVCCM inateswa na siasa za makundi na kuitaka itumie muda wake mwingi kutatua matatizo yake.

“Sasa tukianza kulumbana hapa, tutakuwa tunadhihirisha siasa za makundi. Kwa sababu kuna kauli ambazo ukiziangalia, unajua kabisa hizi zinatokana na kuteswa na siasa za makundi tu na hakuna jambo lingine,” Sitta alikaririwa akisema jana akiwa jimboni kwake Urambo.
“Tumemsikia Sitta akisema vijana tuna matatizo … kwa hiyo hatuwezi kukaa na walezi wenye matatizo. Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa imekaa kikao cha dharura leo (jana) asubuhi, na kuamua kumvua nafasi yake ya Mlezi wa Vijana wa Mkoa,” alisema Kamoga.
Katika mazungumzo yake kwa simu na , Kamoga alisema kutokana na hatua hiyo, wanapeleka taarifa yao kwa uongozi wa UVCCM Taifa kwa hatua zaidi za utekelezaji, lakini wameona ni vyema kuanza kutekeleza kwa vitendo Azimio la Dodoma, kwa sababu wanaamini Sitta ni mtu mwenye akili timamu.
“Tunaamini Mheshimiwa Sitta atatuelewa katika uamuzi huu, kwa sababu hawezi kuongoza watu wasio na akili. Tunaamini mchango wake unatosha sasa, kwa sababu kama ana jambo, alipaswa kulieleza katika vikao husika. Kwa hiyo, tunatekeleza Azimio la Baraza Kuu la kutaka viongozi watumie vikao kuzungumzia masuala ya chama,” alifafanua Mwenyekiti huyo wa UVCCM.
Sitta amekuwa Mlezi wa Vijana wa Mkoa wa Tabora tangu mwaka 2003 na muda wake ulimalizika mwaka 2008, lakini uongozi mpya wa Vijana wa Mkoa ulipoingia madarakani, uliamua aendelee na wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ambacho kingemalizika 2013.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)