PART 2 YA AJALI YA BASI LA OSAKA ILIYOTOKEA MOROGORO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

PART 2 YA AJALI YA BASI LA OSAKA ILIYOTOKEA MOROGORO

Basi la kampuni ya Usaka lenye namba za usajili T 481 BFJ  lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea Dar es Salaam, likiwa limepinduka baada ya kuligonga kwa nyuma lori aina ya Fusso lenye namba za usajili T 873 ALA lililokuwa likitokea Ifakara.


 




NA DUNSTAN SHEKIDELE,GPL MOROGORO
MZIMU wa ajali umeendelea kuutesa mkoa wa Morogoro, ambapo leo majira ya asubuhi basi la kampuni ya Usaka lenye namba za usajili T 481 BFJ lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea Dar es Salaam, leo asubuhi limegongana na lori aina ya Fusso lenye namba za usajili T 873 ALA lililokuwa limebeba shehena ya mchele likitokea Ifakara.

Watu walioshuhudia ajali hiyo, iliyotokea eneo la Maseyu walidai kwamba basi hilo liligonga Fusso kwa nyumba na kupinduka.  Pia, askari aliyekuwepo eneo la tukio aliueleza mtandao huu kwamba katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha na kwamba watu 27 wamejeruhiwa na watatu wakiwa wameumia vibaya sehemu za kichwani.

Hii imetokea baada ya ajali nyingine mbaya iliyotokea Mikumi mkoani hapa usiku wa Jumatatu wiki hii ambapo wasanii 13 wa kundi la Five Stars Modern Taarab walikufa na wengine wanane kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages