Jenerali Yakubu Gowon.
JE, unaifahamu njia ambayo Nigeria, moja ya nchi maarufu barani Afrika imeipitia baada ya kupata uhuru wake mwaka 1961 hadi sasa wakati wa utawala wa Goodluck Jonathan?
Nigeria ilipata uhuru Oktoba Mosi, 1960 kutoka kwa Waingereza ikiongozwa na Waziri Mkuu, Alhaji Sir Abubakar Tafawa Balewa aliyekuwa mtendaji mkuu wa serikali.
Novemba 16, 1960 raia mwingine wa Nigeria, kwa mujibu wa katiba, Dr. Nnandi Azikiwe akawa Gavana Mkuu wa shirikisho la nchi hiyo la majimbo matatu, Kaskazini, Mashariki na Magharibi. Lagos ukawa mji mkuu huku kila jimbo likiongozwa na waziri mkuu ambaye pia alikuwa gavana.
Oktoba Mosi, 1963 Nigeria ikawa jamhuri ya shirikisho, ikamaliza uhusiano na utawala la Uingereza lakini ikaendelea kuwa katika Jumuiya ya Madola iliyokuwa chini ya Uingereza. Hivyo, cheo cha Gavana Mkuu wa nchi hiyo kikabadilishwa na kuwa rais.
Mara vurugu za wanajeshi zikaanza kwani Januari 1966, kundi la maofisa wa jeshi likiongozwa na Jenerali Johnson Aguiyi-Ironsi (pichani) likaiangusha serikali, likamuua Waziri Mkuu, Alhaji Sir Abubakar Tafawa Balewa na Jenerali Johnson Aguiyi-Ironsi akawa mkuu wa nchi.
Mnamo Julai mwaka huo huo, kundi la maofisa wa jeshi kutoka kaskazini mwa nchi hiyo likaasi na kumuua Jenerali Ironsi, likamteua Mnadhimu wa Jeshi, Jenerali Yakubu Gowon kuwa mkuu mpya wa nchi.
Ni wakati wa utawala wa Gowon ambapo vita vya kutaka kujitenga kwa Jimbo la Biafra vilitokea kusini mwa nchi hiyo. Jina la Gowon lilitumika kiutani kuwashauri watu wa Nigeria waendelee kuishi chini ya Nigeria moja.
Utani wenyewe ulitokana na kilichodaiwa kuwa, kirefu cha neno G.O.W.O.N ni Go On With One Nigeria!
Miaka tisa baadaye, 1975, Jenerali Yakubu Gowon naye alipinduliwa na Jenerali Murtala Mohammed ambaye akawa mkuu wa nchi hiyo hadi alipouawa mwaka 1976, yaani mwaka mmoja baadaye.
Nafasi ya Murtala ilichukuliwa na Jenerali Olusegun Obasanjo mwaka huo huo wa 1976.
Wakati matukio ya utawala wa kijeshi yakiendelea, mwaka 1979 nchi hiyo ikaanzisha katiba kama ya Marekani, kukawa kuna rais, baraza la seneti na bunge la wawakilishi.
Mwezi Oktoba 1979, miaka zaidi ya 13 ya utawala wa kijeshi, Nigeria ikarejea utawala wa kidemokrasia ambapo Chama cha National (NNP) kilishinda katika uchaguzi na Alhaji Shehu Shagari akawa rais.
Hata hivyo, baada ya miaka kama minne, yaani mwaka 1985, jeshi likarejea na kuiangusha jamhuri ya pili ya nchi hiyo, yaani utawala wa pili wa kiraia ambapo Meja-Jenerali Muhammadu Buhari akawa kiongozi.
Jeshi halikukomea hapo, Agosti 1985, Jenerali Buhari naye alitoswa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Jenerali Ibrahim Babangida aliyechukua ‘ulaji’.
Hata hivyo, mwaka 1983, Jenerali Babangida akaachia ngazi mnamo Agosti kwa serikali ya muda ya kiraia chini ya Ernest Shonekan.
Lakini, Novemba mwaka huo huo, Jenerali Sani Abacha akatwaa madaraka kutoka kwa Shonekan na kuwa rais. Yeye naye hakudumu, Juni 8, 1998 alikufa ghafla, ikiwa ni miaka ipatayo sita hivi baadaye.
Kifo cha Abacha kilitoa ulaji kwa Meja-Jenerali, Abdulsalam Abubakar.
Katika mlolongo huo ambao raia walikuwa hawana chao kwa wamiliki bunduki na mabomu, Meja-Jenerali Abubakar naye akaachia ngazi Mei 1999 kwa mtu aliyewahi kuwa mkuu wa nchi wa kijeshi, Jenerali Olusegun Obasanjo aliyerejea akiwa katika nguo za kiraia baada ya uchaguzi.
Mambo yakaanza kwenda kistaarabu ambapo mnamo Mei 2007 raia Alhaji Umaru Yar’Adua, akachukua nafasi hiyo kutoka kwa Obasanjo na kuwa mtu wa 13 kuwa mkuu wa taifa hilo ambalo huenda ni maarufu zaidi kuliko nchi zingine za Afrika, ukiachilia mbali Afrika Kusini na labda Misri.
Yar’Adua akaiongoza nchi hiyo hadi alipofariki dunia Mei 5, 2010 na nafasi yake kuchukuliwa kistaarabu na makamu wake, Goodluck Jonathan ambaye akawa kiongozi wa 14 wa nchi hiyo tangu uhuru.
Kwa ulinganisho tu, wakati Jonathan akiwa mkuu wa nchi wa 14 wa Nigeria iliyopata uhuru mwaka 1960, Tanzania ilikuwa imefikisha wakuu wanne tu tangu kupata uhuru wake mwaka 1961!

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)