MASHINDANO YA KOMBE LA UNGULIWA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MASHINDANO YA KOMBE LA UNGULIWA LEO

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sasiq, akisalimiana na Mchezaji wa Taswa Fc, Muhidin Sufiani A.K.A Sufianimafoto, kabla ya kuanza kwa mtanange wa ufunguzi wa Mashindano ya Kombe ka Kamanda Kova, yaliyofunguliwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru.
Kikosi cha TASWA Fc, kikipiga picha ya pamoja na Mdhamini wa mashindano hayo, Rais wa RBP Oil, Rahma Al-Kharus, kabla ya kuanza mtanange huo.Kikosi cha Polisi Jamii kikiwa katika picha ya pamoja.
Timu mbalimbali zinazoshiriki mashindano hayo zikiingia uwanjani kwa Maandamano yaliyofanyika leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kamanda Kova ambayo yatazikutanisha timu za Kijeshi na zile za Kiraia. katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika mapema asubuhi ya leo, timu ya Polisi Jamii imeweza kuibuka kidedea kwa mabao 3-0 dhidi ya timu ya wanahabari ya TASWA Fc.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages