Mabomu Yamerindima Mbarali - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mabomu Yamerindima Mbarali

 
Ndugu Zangu,
Ni mabomu ya kutoa machozi, juzi na jana.

Tafsiri yangu; hali bado si shwari Mbarali. Hata jana mchana mchana nimeongea na walio Mbarali, wameniambia, kuwa jana FFU waliingia Ubaruku, wamerusha mabomu ya kutoa machozi. Wamewapiga na kuwajeruhi raia na hata kufanya uharibifu wa mali pamoja na uporaji pia, ingawa hali ikarudi kuwa shwari na watu wanaendelea na shughuli zao.

Kiini cha mgogoro wa raia na dola kule Mbarali kinabaki kuwa ARDHI na mgawanyo wa RASILIMALI za wananchi kupitia yaliyokuwa mashamba ya wananchi ya Mbarali. Kuyauza mashamba hayo kwa wawekezaji ambako hakukufuata matakwa ya wananchi kutabaki kuwa kero kubwa mpaka hapo litakapopatikana jawabu kubalika na walio wengi, wananchi.

Na hatari ya mgogoro wa Mbarali ni kuenea kwa chuki baina ya wenyeji wa asili na ndugu zao Waburushi. Naiona pia, hatari ya mgawanyiko na hata kupelekea mapambano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wakazi wa miji ya Rujewa na Ubaruku kutokana na kujitokeza kwa tofauti za kimisimamo katika mgogoro huu.

Hilo la mwisho likitokea, basi, litakuwa na madhara makubwa sana. Tuna kila sababu na uwezo wa kuepusha machafuko makubwa Mbarali kama kweli tuna dhamira za dhati za kusimamia haki na kutanguliza maslahi ya walio wengi.

Serikali ianze kwanza na kuwawajibisha wale wote waliotufikisha hapa.

Maggid,
Iringa.
http://mjengwa.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages