Msanii wa maigizo, Mzee Small (katikati) akimkabidhi Tuzo Man Water, kwa niaba ya 20 Pacent, aliyeibuka kidedea katika Kategoli ya Wimbo bora wa Afro Pop, (kulia) ni Bi Chau. Msanii huyo jana katika onyesho la kutoa tuzo hizo za 'Tanzania Kili Music Awards' alifunika na kuweza kujizolea jumla ya tuzo tano na kuufanya ukumbi kuzizima kwa makelele ya kushangilia kila alipotajwa jina kushiriki katika Kategoli fulani. Hata hivyo msanii huyo hakuweza kuhudhulia onyesho hilo kutokana na kupata safari ya ghafla kulingana na maelezo ya mwakilishi wake, ambaye pia ni Producer wake Man Water.
CP...Cpwaaa Akiwashukuru Wadau Wote Kwa Ujumla Katika Kuhakikisha Anashida
Lady Jay Dee nae ni mmoja wa wasanii waliobuka na tuzo nyingi Mashabiki waliohudhulia onyesho hilo, wakishangilia baada ya kutajwa jina la 20 Pacent.
Jay Moe (wapili kushoto) JBC na Producer, wakipozi na tuzo zao baada ya kutwaa tuzo hizo jana usiku.
Mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete (kulia) akimkabidhi tuzo ya Wimbo bora wa Raggae Dance hall, msanii C-Pwaa. Kushoto ni mchezaji wa Simba, Mussa Hassan 'Mgosi'.
Mwenyekiti wa Kamati ya ushindi ya timu ya Taifa, Rahma, naye alikuwepo ukumbini humo akipata raha kamili.
Waziri wa habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, Angetile Osiah.
Mtangazaji wa redio Times, akimkabidhi tuzo msanii Barnaba, baada ya kuibuka kidedea katika kategoli ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba. katikati ni Mzee wa Planet Bongo, Dullah.
Patricia Hirary, akimkabidhi tuzo, Mpoki baada ya kuibuka kidedea katika Kategoli ya Wimbo bora wa Asili na wimbo wake wa Shangazi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)