Baadhi ya wananchi waliofika eneo la ajali ya basi dogo lililokuwa limewabeba wasanii wa taarab wa kikundi cha Five Stars Modern Taarab wakipekua vitu mbalimbali ndani ya basi hilo usiku muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea katika kijiji cha Doma, Mvomero, Morogoro. Picha na John Nditi
--
UKAIDI wa dereva wa basi dogo aina ya Coaster umesababisha vifo vya wasanii 13 wa kikundi cha taarabu cha Five Stars Modern Taarab cha Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa dereva huyo aliyetajwa kwa jina moja la Chala alikaidi ushauri wa abiria waliomtaka apunguze mwendo, akaligonga lori la mizigo lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara kuu ya Iringa – Morogoro katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Basi hilo namba T 351 BGE lililokuwa katika mwendo mkali liligonga lori aina ya Scania namba T 848 APE lililokuwa na tela namba T559BDL lililokuwa limesheheni mbao na kuegeshwa katika kijiji cha Doma, wilayani Mvomero baada ya kuharibika.
Katika ajali hiyo watu 12 walikufa papo hapo na mwingine aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)