TUJIULIZE KWANINI MAJANGA JESHINI YAMEKITHIRI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TUJIULIZE KWANINI MAJANGA JESHINI YAMEKITHIRI

 
Tumshukuru Mungu kwa kutupa uhai leo huku tukimuomba aziweke roho zao mahali pema peponi  waliokufa kwa mabomu wiki iliyopita huko Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. Tunaamini wote waliokufa ambao tulikuwa tukiwapenda sana, Mungu amewapenda zaidi.

Baada ya kusema hayo, sasa tukumbushane tu kwamba katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) tunalolitegemea kwa ulinzi wetu, kumekuwa na matukio mengi ambayo yanapaswa kuitwa ni majanga.

Ndugu zangu, mtu mwenye kufikiri ni lazima ajiulize, nini kinasababisha haya majanga kutokea ndani ya jeshi hili mara kwa mara?

 Wakati baadhi ya watu waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wameanza harakati za mazishi ya wapendwa wao ambao walipatwa na janga la milipuko hiyo ya mabomu ya jeshi katika kikosi cha 511, tutafakari kwa pamoja matukio yafuatayo kisha tuchekeche ubongo kuona nani wa kulaumiwa.

Ndugu zangu, kweli inawezekana hizi ajali ni za bahati mbaya lakini kinachosumbua wananchi wengi hasa wenye uwezo wa kutafakari na kujenga hoja kwa kutazama mwenendo wa mambo ndani ya nchi yao, ni kujirudia kwa tukio hili la kulipuliwa watu na mali zao kwa kipindi kifupi sana. 
Kwa Stori Zaidi  <<<<< BOFYA HAPA >>>>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages