TANESCO YASHINDWA KUTEGUA KITENDAWILI CHA MGAO WA UMEME TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANESCO YASHINDWA KUTEGUA KITENDAWILI CHA MGAO WA UMEME TANZANIA


 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco,  Injinia, Felchesmi Mramba,Akizungumza na waandshi wa habari ,kwenye makao makuu ya Tanesco,Ubungo Jijini Dar es Salaam,  alisema, mafuta yameshanunuliwa  na yameanza kuwasili IPTL, ili kuzalisha kiasi hicho cha megawati za umeme kwa siku.
 Waandishi hawa wakakaa 'high table' na kusema, "ndugu waandishi wa habari, tumewaita leo kuzungumzia  hali ya mgawo wa.... lakini bahati mbaya tumechelewa kuanza... Haya ulizeni maswali...(Kicheko)
---
Shirika la Umeme nchini, Tanesco, sasa limenunua mafuta ya kuendeshea mtambo wa umeme wa IPTL uliopo, Tegeta, Dar es Salaam, ili kuzalisha megawati 80 kwa siku, ikiwa ni moja ya hatua zake kujaribu kupambana na mgawo wa umeme ambao shirika hilo limekiri kuwa unalipunguzia heshima kwa umma.  Akizungumza na waandshi wa habari , kwenye makao makuu ya Tanesco,Ubungo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco,  Injinia, Felchesmi Mramba,(Pichani), alisema, mafuta yameshanunuliwa  na yameanza kuwasili IPTL, ili kuzalisha kiasi hicho cha megawati za umeme kwa siku.

      "Hii itapunguza  mgawo wa umeme kwa sasa kwa megawati zipatazo 70", alisema Injinia huyo ambaye alifuatana na Meneja Uhusiano wa Shiruika hilo, Badra Masoudi (kulia) na kuongeza "tunatarajia kwamba msimu wa mvua za masika utaanza punde, na hii itafanya uzalishaji wa umeme katika mitambo ya maji kuongezeka na hivyo kuliondoa tatizo hilo kwa sasa.

  "Pia Shiruka linawasiliana na serikali kuangalia uwezekano wa kupata mit ambo ya dharura ili kukabiliana na hali inayoweza kujitokeza endapo mvua za masika zitakuwa chini ya wastani unaotarajiwa", akasema Injinia Mramba.
     Akasema, uongozi wa Tanesco unawaomba radhi sanaaaa, wananchi kutokana na usumbufu mkubwa unaotokana na adha ya mgawo huo wa umeme na pia Shirika linawasihi  wananchi kushirikiana na shirika hilo, na kuwa  watulivu katika kipindi hiki kigumu cha upungufu wa umeme.

  "Tunaahidi kwamba tutafanya kila jitihada kurekebisha mapungufu balimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hapa na pale katika utekelezaji wa zoezi hili la mgawo hasa kudhibiti matukio ya dharura yanayofaya ratiba zisifuatwe kama zilivyopangwa", akamaliza..

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages