SEMINA YA WATEULE TUZO ZA MUZIKI YAFANA DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SEMINA YA WATEULE TUZO ZA MUZIKI YAFANA DAR

George Kavishe, akiongea jambo katika hafla hiyo.
SEMINA ya Wateule wa Tuzo za Kili Music Awards 2011 jana ilifana katika ukumbi wa Paradise Hotel, jijini Dar es Salaam, ambapo wasanii hao walikutana na uongozi mzima ulioandaa shughuli hiyo na kubadilishana mawazo.
 
Angelo Luhala, akizungumza na wasanii wa semina hiyo.
Akiongea na wateule hao, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema amelazimika kuwaalika mapema wateule hao ili kuchanganua baadhi ya makundi (category) yaliyopangwa kimakosa ili kuzuia malalamiko kutoka kwa washiriki.

Aidha mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Angelo Luhala, alisema wito huo wa wasanii ni njia moja ya kuwapa fursa ya kupendekeza marekebisho kabla ya siku ya utoaji tuzo hizo.


Msanii wa kundi la Orijino Komedi, Sylvester Mujuni ‘Mpoki’ aka Bepari la Kihaya (kulia), akibadilishana mawazo na msanii wa ‘Hip Hop’,  Joh Makini, kwenye hafla hiyo.

 
Msanii wa mashairi, Mrisho Mpoto (kulia), na msanii mwenzake, Kassim Mganga, wakifuatilia baadhi ya makundi kama yalivyoandikwa.

 
Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, akipata matunda muda mfupi kabla ya kuingia kwenye kikao hicho.

 
Msanii wa Hip Hop, Faridy Kubanda (Fid Q) akihoji jambo fulani katika hafla hiyo.

 
Ali Kiba naye hakuwa nyuma kuuliza swali kwenye kikao hicho.

 
Kiongozi wa bendi ya African Stars International (Twanga Pepeta) Luiza Mbutu (katikati), akiwa kwenye picha na baadhi ya wanamuziki waliyojiengua kwenye bendi hiyo ambao ni Kalala Junior (kulia), na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’ (kushoto), nyuma yao (kulia), ni Rapa wa Twanga Pepeta, Said Msafiri Sayai (Msafiri Diouf) na Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu, Hamisi Dakota.

 
Baadhi ya wasanii waliohudhuria mchakato huo wakifuatilia zoezi hilo kwa ujumla.

 
Mzee Yusuf (kushoto), akiwa na Kassim Mganga ambaye ameshikilia magongo yake.
Picha/Habari: Musa Mateja/GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages