MWISHO ATUA DAR NA MERYL - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWISHO ATUA DAR NA MERYL

 
Na Erick Evarist
Mwakilishi wa Taifa la Tanzania katika Kinyang’anyiro cha Big Brother Africa ‘All Stars’ 2010, Mwisho Mwampamba ametua Bongo akiambatana na mchumba’ke Meryl Shikwambane, raia wa Namibia, Amani limeinyaka.

Kwa mujibu wa     Mtandao wa Bongo Starslink, Mwisho na Meryl walitia maguu jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii wakitokea Namibia kupitia Afrika Kusini ‘Sauz’.

Mtu wa karibu wa familia ya Mwisho aliyeongea na Amani juzi alisema kuwa, staa huyo alitarajiwa kumpeleka Meryl mji kasoro bahari ‘Moro’ kwa ajili ya utambulisho rasmi kama ilivyokuwa upande wa mrembo huyo huko Namibia.

Baada ya kuzitia kibindoni habari hizo, Amani lilimuinulia mkonga wa simu Mwisho ili kupata undani wa ishu hiyo ambapo jamaa alitoa lugha chafu isiyoandikika gazetini.

Hivi karibuni Mwisho alitimkia nchini Namibia ambapo alikwenda kutambulishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mchumba wake huyo.

Mwisho na Meryl ni wachumba ambao walikutana katika Jumba la BBA ambapo waliingia kwenye uchumba kama ilivyokuwa kwa mshiriki mwingine wa Tanzania, Elizabeth Gupta aliyeolewa na mwenzake wa kutoka Nigeria, Kevin Chuwang.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages