Musa Mateja na Shakoor Jongo
Mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, kinachorushwa hewani kupitia Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam, Khadija Shaibu ‘Dida’ (pichani), juzikati alinusurika kufa baada ya gari lake kugongana na gari dogo aina ya Nissan March lenye usajili namba T353 BFG.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Januari 31 mwaka huu, eneo la Makumbusho Kijitonyama jijini Dar es Salaam, wakati Dida alipokuwa akitokea nyumbani kwake kuelekea kwenye saluni iliyopo katika jengo la Green Acres Saloon lililopo maeneo hayo.
Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilisema kuwa mtangazaji huyo akiwa kwenye harakati za kuingia kuelekea katika jengo hilo, ghafla lilitokea gari lililokuwa ‘likitanua’ barabarani na likamvaa ubavuni ambapo gari lake ililiharibika vibaya kwa kupondeka.
“Dida alishuka ndani ya gari na kulikagua, baada ya kuona madhara aliyotokea, alihamaki na kuanza kumkoromea kijana aliyemgonga.
“Lakini baadaye walifikia muafaka ambapo jamaa huyo alikubali kwenda kumtengenezea gari lake,” kilisema chanzo hicho.
Dida alipotafutwa na kuulizwa kuhusu ajali hiyo alithibitisha kutokea akaongeza: “Namshukuru Mungu kwa kuwa sikuumia, ni mapenzi yake ndiyo yameniweka salama.
“Kwenye gari lao kulikuwa na akina baba wawili na baada ya kutokea ajali hiyo walijadiliana wanitoe vipi, tulimalizana kwa kukubaliana kuwa watanitengenezea gari langu.”

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)