EPHRAIM KIBONDE WANTED BY UDSM STUDENTS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

EPHRAIM KIBONDE WANTED BY UDSM STUDENTS

Mtangazaji Wa Clouds Fm Epharaim Samson Kibonde.
  AFUNGA UKURASA WAKE WA FACE BOOK
Mmoja wa wanaharakati wa Chuo hicho, Gwakisa, akiwahutubia wanafunzi wenzake kuhusu dhamila yao ya kumsaka Kibonde.

Na Sufianimafoto, Reporter jijini

MTANGAZAJI wa redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Ephraem Kibonde, akepigwa wanted na wanafunzi wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam kwa kile walichodai kudhalilishwa na mtangazaji huyo katika moja ya vipindi vyake vya redio.
Wanafunzi hao wamechukua hatua hiyo ya kuanza kumtafuta Mtaa kwa Mtaa, baada ya kumsikia katika Kipindi chake akizungumzia kuhusu mgomo wao na kusema maneno yasiyostahili kimaadili kuhusu wanafunzi hao.
Imeelezwa kuwa juzi kundi la wanafunzi kama miamoja lilizuiliwa na askari wakati likiwa katika harakati za kuelekea nyumbani kwa mtangazaji huyo maeneo ya Mabibo.
Hata hivyo walisikika baadhi ya wanafunzi hao wakati wakiwa chuoni hapo jana kuwa bado lengo lao la kufika katika makazi ya mtangazaji huyo lipo pale pale na kwamba hivi sasa wameamua kukodi Kosta nne kwa ajili ya kupakia wanafunzi kuelekea kwa mtangazaji huyo, zoezi ambalo litatekelezwa muda wowote kuanzia jana.
Aidha alisikika mmoja wa Viongozi wa wanafunzi hao aliyepanda jukwaani jana mbele ya Waziri wa Elimu, Rich Mwita na kutangaza kuwa hivi sasa zoezi hilo la kumfuatilia mtangazaji huyo wamelisitisha kwanza ili kutoa fulsa kwa viongozi wa Serikali kuwafanyia kazi zaidi kuhusu madai yao ya kupata Sh. 10,000 badala ya 5,000.
“Kwa sasa tumeamua kwanza kuachana na mpuuzi huyu mmoja ili tusijewashawishi viongozi kutuona kuwa sisi ni wakorofi kwa kushika mambo mawili mawili, hivyo kwa sasa tunadili zaidi na suala letu na madai huyu jamaa wala hatusumbui tunauwezo wa kumpata muda wowote kutikihitaji” alisema Rich.
Naye Gwakisa alisikika akisema kuwa mtangazaji huyo, alisikika redioni akisema kuwa dada zao wamekuwa wakijiuza kwa mashefa na watu kadhaa ili kupata fedha za kukidhi mahitaji yao baada ya kukosa fedha za matumizi.
Aidha imeelezwa kuwa baada ya wanafunzi hao kumsaka na kumkosa, waliamua kuanza kumtafuta katika ukurasa wa 'FACE Book', ambapo kila aliyeingia katika ukurasa huo alikuwa akitoa dukuduku lake na kumtusi kiasi cha kumfanya Kibonde aamue kufunga ukurasa wake huo kuanzia jana
                     Wanafunzi hao wakiwa katika harakati za maandamano chuoni hapo jana.



1 comment:

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages