Na Raymond Kaminyoge
ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, amejitangazia uadalifu akisema uchunguzi wa kashfa ya rada uliofanywa na Taasisi ya Kuchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza , umegundua hahusiki, lakini alikimbia maswali ya waandishi.
Wakati Chenge maarufu mzee wa vijisenti, akitumia mkutano wake na waandishi wa habari jana kujitangazia uadilifu huo, Ikulu kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, imeshikwa na ganzi kuthibitisha au kukaa uadilifu huo.
Chenge mwenyewe alisema:, " “Mimi ni muadilifu. nimefanya kazi katika awamu zote nne za uongozi wa nchi yetu..., hata nilipojiuzulu sikuwa na hofu wala mashaka ya kupoteza kazi.”
Chenge akirejea na kujivunia historia ya utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kufanya kazi wakati wa Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, alisisitiza uadilifu wake akisema:, "Kwa kuwa nilijiamini sikutenda kosa lolote katika kashfa hiyo ya rada nilisema iko siku ukweli utajulikana.”
Mbunge huyo wa Bariadi Magharibi, alisema alitajwa kwenye kashfa ya rada iliyolitikisa Bunge la Uingereza, baada ya SFO kubaini alikuwa amehifadhi takribani Sh1.2 bilioni kwenye akaunti yake ya benki moja kisiwani Jersey, ambazo baadaye aliziita vijisenti.
SFO ilibaini akaunti hiyo wakati ikifuatilia mzunguko wa fedha zilizonunua rada. “ Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa walikamilisha uchunguzi wao na kugundua kwamba hakuna ushahidi ulionihusisha na rushwa, uchunguzi umefanyika Uingereza na imeonekana sihusiki,”alizidi kujisafisha
Kwa mujibu wa Chenge, makubaliano yaliyofikiwa mahakamani hapo ni kwamba SFO, haitamshtaki mtu yoyote kufuatia uchunguzi huo wa rada. “ Pia hakutakuwa na uchunguzi wala mashtaka ya aina yoyote kwa uongozi wa BAE Systems unaohusu mambo ya kibiashara yaliyofanywa kabla ya Februari 5, 2010,”alizidi kuanika hukumu hiyo huku akigoma kujibu maswali ya waandishi wa habari.
Chenge mwanasiasa na mwanasheria mwenye kupenda kutumia maneno ya mzaha alisisitiza:, “ Kwenye ukweli uongo hujitenga, SFO na Takukuru wamefanya uchunguzi wa kina na matokeo yamedhihirisha mimi ni mtu safi.”
Katika kutaka kujijengea imani kwa umma, Chenge aliwaomba Watanzania kuacha kushabikia mambo kabla hawajayafanyia utafiti wa kina. ``Rada ilinunuliwa na Serikali kwa manufaa na ulinzi wa nchi yetu na ununuzi wake ulizingatia sheria na taratibu zote za Serikali,’’alifafanua.
Sakata la rada limekuwa likitikisa Bunge na Serikali ya Uingereza, hadi wakati flani kumfanya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa nchi hiyo, Clare Short kujiuzulu huku aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Robin Kook, akimshambulia aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Tony Blair baada ya kuidhinisha BAE Systems kuuza rada hiyo kwa Tanzania wakati ni nchi maskini.
Kwa upande wa hapa nchini, sakata hilo limekuwa likitikisa ambalo hivi karibuni Chenge alitoa kauli kama hiyo wakati akitangaza kuwania kiti cha uspika wa Bunge, lakini baadaye Uingereza, ikasema jalada hilo halikuwa limefungwa.

SOURCE: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)