Daniel Mjema, Moshi
WAFANYAKAZI kadhaa wa Benki ya CRDB Limited matawi ya Vijana Jijini Dar es Salaam na Marangu mkoani Kilimanjaro, wanashikiliwa polisi kutokana na wizi wa Sh400 milioni zilizohamishwa kwa njia ya mtandao.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mfanyabiashara wa Marangu ambaye ni mkandarasi (jina tunalo) ambaye alifanikiwa kutoa Sh35 milioni kabla ya uongozi wa benki kushitukia ‘dili’ hiyo na kuisimamisha akaunti hiyo.
Habari za uhakika ambazo Mwananchi inazo, zimedai kuwa mfanyabiashara huyo aliwalaghai watunza fedha wa tawi la CRDB Marangu kuwa fedha hizo ametumiwa ili kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya lami wilayani Rombo.
Hata hivyo muda mfupi baada ya kutoa kiasi cha Sh35 milioni, uongozi wa CRDB Dar es Salaam ulishtukia dili hilo na jitihada za kuokoa fedha hizo Sh400 milioni zisitolewe zote zilikaishia kuambulia Sh365 milioni.
Habari hizo za uhakika zimefafanua kuwa baadhi ya wafanyakazi wa CRDB tawi la Vijana Jijini Dar es Salaam wanadaiwa kuonyesha kwenye mtandao wa benki kuwa mfanyabiashara huyo aliingiziwa fedha taslimu Sh400 milioni.
Lakini uchunguzi wa Mwananchi na wa CRDB Jijini Dar es Salaam uligundua baadaye kuwa hakuna mteja yeyote aliyekuwa amefika tawi la Vijana na kuingiza kiasi hicho cha fedha bali ni ‘mchezo’ uliochezwa ndani ya Benki.
Inadaiwa kuwa ‘dili’ hilo la wizi wa kimataifa wa kutumia mtandao wa kompyuta lilifanywa Desemba 29, mwaka jana na baada ya fedha zote kutolewa, wafanyakazi hao wa CRDB wangeondoa ingizo hilo kwenye kumbukumbu za Tawi la Vijana.
“Ambacho kingetokea ni kwamba mwisho wa siku CRDB ndio wangekuwa wameibiwa kwa sababu Tawi la Marangu, mteja anaonekana ameingiziwa fedha, lakini Vijana hiyo transaction (ingizo) lingeondolewa,” Mwananchi limedokezwa.
Habari zinadai kuwa wafanyakazi wawili wa Tawi la Marangu pamoja na mfanyabiashara huyo walisafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam juzi ili kuunganishwa na wafanyakazi wengine wa CRDB Tawi la Vijana wanaoshikiliwa polisi.
Ingawa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Yusuph Ilembo, hakuweza kupatikana jana kuelezea tukio hilo baada ya simu yake kutopatikana, lakini Mkurugenzi wa CRDB Mkoa wa Kilimanjaro, Francis Mollel alithibitisha tukio hilo.
“Ni kweli kuna tukio kama hilo, lakini ni jambo lililoanzia huko Tawi la Vijana Dar es salaam na wafanyakazi wetu Marangu ni 'very innocent' (hawakujua lolote) maana mtu kaingiziwa fedha taslimu unafanyaje?”alihoji Mollel.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa mfanyabiashara huyo baada ya kuingiziwa fedha taslimu,alitoa Sh35 milioni kwa kuandika hundi ambayo kwa hali ya kawaida isingekuwa rahisi mtu kugundua ingizo hilo lilikuwa ni haramu.
Kwa mujibu wa Mollel, wafanyakazi wake tawi la Marangu waliohusika kushughulikia malipo hayo walikamatwa na kuhojiwa polisi kabla ya kusafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam kama utaratibu wa kawaida wa upelelezi.
Mwaka jana, Mwananchi liliwahi kuripoti kuhusu namna mabenki mbalimbali nchini yanavyolizwa mabilioni ya shilingi kila mwaka kutokana na wizi kwa njia ya mtandao na watuhumiwa mbalimbali hivi sasa wako mahakamani kwa tuhuma hizo.
Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai nchini(DCI), Robert Manumba aliwahi kukaririwa akisema jeshi hilo limejipanga vilivyo kukabiliana na wizi huo kwa njia ya tekinolijia ingawa inaonekana polisi na baadhi ya benki zinazidiwa ujanja.
Habari za uhakika kutoka kwa chanzo ndani ya benki moja nchini, zilidokeza kuwa matukio mengi ya aina hiyo humalizwa ndani kwa ndani kutokana na kuwahusisha baadhi ya wafanyakazi wanaotumia tekinolojia ya hali ya juu.

Source: Mwananchi Newspaper
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)