WASANII WA FILAMU TANZANIA WATUNUKIWA TUZO ZAO LEO NA FILAMUCENTRAL - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASANII WA FILAMU TANZANIA WATUNUKIWA TUZO ZAO LEO NA FILAMUCENTRAL

Mwakilishi wa tuzo za Filamucentral,Myovela Mfwaiza akizungumza mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla fupi iliyofanyika leo mchana kwenye hotel ya Tamal,Mwenge jijini Dar.Pichani nyuma ni Steven Kanumba.
Mmoja wa Waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini,Steven Kanumba akitoa shukurani kwa waandaaji wa tukio hilo mara baada ya kukabisdhiwa tuzo zake.Kanumba ameibuka na tuzo ya Muigizaji bora wa Filamu pamoja na Mtayarishaji bora filamu 2010.
Mgeni rasmi,ambaye pia ni Mkurugenzi ZIFF,Prof Martin Mhando akimkabidhi tuzo yake Jenifer Daudi ya Muigizaji bora chipukizi wa filamu 2010,Jenifer ameibuka na tuzo hiyo mara baada ya kuonyesha umahiri mkubwa katika uigizaji kupitia filamu ya This is it pamoja na Uncle JJ za Kanumba.Hafla hii imefanyika mapema leo mchana ndani ya hotel ya Tamal,Mwenge jijini Dar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages