Fredy Azzah
Leo tunaanza mwaka mpya wa 2011, ikiwa ni jana tu tumeupa kisogo mwaka 2010. Mwaka jana ulikuwa na matukio mengi ya kukumbukwa kama taifa. Miongoni mwake yapo ambayo ni makubwa yaliyoadika historia katika taifa letu.
Rashid Kawawa afariki dunia
WATANZANIA waliuanza mwaka 2010 kwa majonzi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe nchini na mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika, Mzee Rashidi Kawawa.
Kawawa alifariki dunia Disemba 31, 2009 saa 3:20 asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo siku hiyo hiyo Rais Jakaya Kikwete alitangaza rasmi kifo cha Mwasisi huyo wa taifa hili.
Ajali mbaya yaua 20 Handeni
Mwaka huu haukuandamwa ajali nyingi za barabarani, ingawa ile iliyotokea Februari 2, na kusababisha vifo vya watu 25 na wengine zaidi ya 52 kujeruhiwa haitosahaulika.
Kinachoifanya ajali hiyo kuwa na historia ya kipekee, ni kupona kwa mtoto wa miaka miwili aliyekuwa akisafiri na baba yake. Baba huyo alifariki dunia.
Ajali hiyo ilihusisha mabasi mabasi mawili ambayo ni Mzuri Transport, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Lushoto na Chatco lililokuwa likitokea Arusha kuelekea Dar es salaam, kugongana uso kwa uso katika barabara ya Segera – Chalinze, Kijiji cha Kitumbi kilicho Handeni, Tanga.
Jerry Muro kizimbani
Februari 5, mtangazaji wa televisheni ya Shirika la Utangazaji (TBC1), Jerry Muro alipandishwa kizimbani akishtakiwa kwa kula njama na kuomba rushwa ya Sh10 milioni.
Muro ambaye ni mwandishi bora wa habari wa mwaka 2009, tuzo aliyoipata kutokana na kuripoti habari zilizofichua rushwa inayofanywa na askari wa kikosi cha usalama barabarani, alipandishwa kizimbani na wenzake wawili ambao inadaiwa alishirikiana nao kutenda kosa hilo.

Kwa Mengine Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)