Kikosi cha Taifa Stars.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars inaingia uwanjani leo kumenyana na Misri bila washambuliaji wake hatari, Athumani Machuppa, na Rashid Gumbo walioachwa Dar es Salaam.
Machuppa anayecheza soka la kulipwa katika Klabu ya Vasalunds IF inayoshiriki daraja la kwanza nchini Sweden ameachwa baada ya majina yake kukosewa kwenye tiketi huku tatizo hilo likimkumba pia Gumbo anayeichezea Simba.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Machuppa alisema anatarajia kuungana na Stars leo kwa ajili ya mechi ya ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Nile dhidi ya wenyeji Misri, itakayopigwa jioni.
“Kuna kosa kidogo lilitokea kwenye tiketi, lakini kila kitu kimerekebishwa hivyo nitaungana na wenzangu kwa ajili ya michuano hiyo,” alisema.
Washambuliaji hao walitarajiwa kuondoka jana, kwenda kwenye michuano hiyo baada ya kuonyesha kiwango cha juu mazoezini.
Stars imewasili mjini Cairo, Misri salama salimini tayari kwa michuano hiyo, huku Kocha Mkuu, Jan Poulsen akiungana nao huko baada ya kuwa nchini mwake, Denmark kwa ajili ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Tunapenda Kuwatakia Taifa Star Ushindi Wa Nguvu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)