Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Anne Makinda akiwa pamoja na Maspika wenzake kutoka katika mabunge ya nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Madola ambao wanaunda Kamati Tendaji. Maspika hawa wanakutana katika kisiwa cha Isle of Man kilichoko chini ya utawala wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kuandaa mkutano wa wanachama wote utakaojadili mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupanda kwa bei za vyakula ulimwenguni. Kikao hicho kilichoanza tarehe 12 kitakamilika tarehe 15 Januari 2011. Spika Makinda atarejea nyumbani tarehe 16 Jan. 2011. Hapa maspika wako kwenye tafrija iliyoandaliwa kwa heshima yao.
Spika Makinda akiwa na Spika wa India Mhe. Meira Kumar (kati) katika mkutano huo
Maspika wakitembelea maeneo mbalimbali ya kihisoria katika Kisiwa cha Isle of Man Picha na Prosper Minja - Bunge
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)