Zile fainali za kumtafuta Shujaa wa Mwaka zimefikia tamati usiku huu na Bw. Paul Luvinga wa Sinza Dar ameibuka kidedea kwa kupata kura nyingi kuliko wenzake akina Bi. Mercy Shayo wa Boma Ngo'ombe Kilimanjaro na Leonard Mtepa wa Mwananyamala Dar. Kwa ushindi huo, Bw. Luvinga amejishindia kitita cha shilingi milioni 7 na Tunzo maalum. Washiriki wenzake kila mmoja kaondoka na kifuta jasho cha shilingi milioni moja. Hafla hiyo imefanyika Paradise City Hotel ya jijini Dar es sasalaam na mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Ajira na Kazi, Mhe. Milton Mahanga. Tunzo hizo ziliandaliwa na TBL kwa kushirikiana na kituo cha Televisheni cha ITV na radio One cha jijini Dar. Pichani ni Bw. Luvinga akionesha tunzo yake kwa waalikwa mara baada ya kukabidhiwa.
Waziri Mahanga akimtangaza mshindi huku akishuhudiwa na vingozi wa TBL, David Minja (Kati) na Fimbo Butallah.
...ni furaha ya ndugu wa Luvinga
Washiriki wa Shujaa wa Mwaka. Kulia ni Leonard, Mercy na Luvinga wakiwa na mfano wa cheki zao.
Mtangazaji wa Radio One ambaye alikuwa MC, Ndyamala (kushoto) akiwa na mgeni rasmi.
Mashujaa wa mwaka. Kutoka kulia; Leonard, Mercy na Luvinga wakiwa katika picha ya pamoja
Ushujaa wa Bw. Luvinga umetokana na kitendo chake cha kuanzisha Maktaba (Library) ya bure mtaani kwake, ambapo wanafunzi wengi hujisomea usiku na mchana, imewasaidia majirani zake na wakazi wa Sinza kujisomea bure, kupitia maktaba hiyo vijana wengine wako vyuo vikuu hivi sasa.
Ushujaa wa Bw. Mtepa umetokana na kumsaidia bibi kizee kutetea haki ya nyumba yake ambayo alikuwa anadhulumiwa. Bibi huyo, ambaye alizaa watoto tisa lakini wote wamekufa isipokuwa mmoja tu, anaishi na vijukuu katika mazingira magumu kule mwananyamala Dar.
Ushujaa wa Bi Shayo umetokana na kitendo chake cha kumsaida jirani yake wa kike anayeishi na virusi vya ukimwi kuendelea kuishi kwa matumaini, kusaidia yatima na kumsaidia kijana aliyevunjika mguu mara tatu.
Bw. Butallah kutoka TBL akifungua rasmi hafla hiyo
David Minja wa TBL akisoma hotuba fupi
Waziri Mahanga akisoma hotuba
Viongozi wa Radio One, Deo Rweyunga (kulia) na Ayoub Semvua wakifuatilia hafla hiyo
waimbaji wa Mpoto Band wakiburudisha wageni waalikwa katika hafla hiyo.
PICHA: Abdallah Mrisho/GPL
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)