Takribani Leo ni siku ya Pili Tokea Matokeo Ya kidato Cha Nne mwaka 2010 yatangazwe na Katibu Mtendaji Wa Baraza La MItihani La Taifa (NECTA) Dk Joyce Ndarichako. Matokeo Ya Mwaka Huu Yanaweza Kuwa Ni Mabaya Kupita Miaka Yote Iliyopita Kwa idadi ya Nusu Asilimia Nzima Kupata division Zero Au Sifuri Kama Ijulikanavyo...Lakini je tuangalie ni nini sababu ya matokeo haya mabaya kupita kiasi kwa asilimia kubwa na kuwa mazuri kwa asilimia ndogo ambayo asilimia ndogo hiyo imetoka kwenye shule binafsi na za seminari..vipi kuhusu shule zetu tulizochangishwa na serikali yaani shule za kata na je wanafunzi wote hawa waliopata dvision three,four na zero tunawapeleka wapi au ndo wote wanakimbilia ualimu? Na Mfano Mzuri Wa Kudhirisha kuwa matokeo ni mabovu kupita kiasi Ni Shule ya NDUNGU ambayo haina division one,two na hata three alama zilizopatikana hapo ni kuanzia division four na zero je watoto hawa tunawapeleka wapi ambao wapo takribani 105 je hawa wote wataenda ualimu?Na watoto hawa wakiwa walimu ni zao gani Linalozalishwa Kutokana Na Walimu hawa waliopata Division Four na Zero?Kwa Hili Serikali Inabidi Ingalie Upya Mpango Mzima Wa Ualimu.Na Kwa Matokeo Haya Tuwalaumu Wakina Nani?Serikali Kupitia Wizara ya Elimu, Necta Wenyewe, Wanafunzi Waliofeli au Walimu? Kwa kuthibitisha hili ebu angalia matokeo ya shule hii mojawapo ya shule za Tanzania NDUNGU BOFYA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA NDUNGU
By Josephat Lukaza
Http://Josephatlukaza.blogspot.com





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)