Na Tullo Chambo
HAKIKA ni majonzi kwa familia ya Wananetiboli na wanamichezo kwa ujumla kutokana na kuondokewa na mshambuliaji mahiri, Neema Emmanuel aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana kutoka Ofisi ya Michezo ya Jeshi la Polisi Tanzania, marehemu Neema alikutwa na mauti hayo katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya ujauzito.

PC Neema, mahiri kwa kutumia mkono wa kushoto, aliwahi kung’ara vilivyo na timu za Polisi Tanga kisha Polisi ya Dar es Salaam ambayo alikuwa nayo hadi sasa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Queens’ alikuwa akimudu vilivyo nafasi za GA na GS, pia alikuwa mahiri katika mpira wa kikapu akiwa na timu yake ya kazini na Mkoa wa Dar es Salaam ‘Dream Teams.
Msiba wa marehemu uko nyumbani kwake Polisi Barracks ambako anatarajiwa kuzikwa leo makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi ameni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)