MIGOMO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU ZINACHANGIWA NA VYUO NA TUME YA VYUO VIKUU (TCU) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MIGOMO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU ZINACHANGIWA NA VYUO NA TUME YA VYUO VIKUU (TCU)

  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, George Nyatega akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam.Picha na Yusuf Badi
 ........................
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeshutumu kile ilichoeleza kuwa ni kugeuzwa jimbo la uchaguzi na baadhi ya watu, kwa kutumia mgongo wake kutoa shutuma bila kuzifanyika uchunguzi, ili wasikilizwe na wanafunzi wa elimu ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, George Nyatega, jana aliwambia waandishi wa habari Dar es Salaam, kwamba Bodi yake imekuwa ikigeuzwa ajenda na watu hao huku ikihusishwa moja kwa moja na migomo ya wanafunzi wakati kasoro nyingi zinachangiwa na vyuo vyao na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Nyatega alisema lengo lake si kujibu tamko la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambao hivi karibuni ulitoa tamko kutaka Bodi ipanguliwe.

Lakini taarifa ya maandishi iliyogawiwa kwa waandishi na pia kuchapishwa katika baadhi ya magazeti jana, Mkurugenzi Mtendaji aliijibu UVCCM kwa kusema imekurupuka kwa kutoa shutuma ambazo hazijafanyiwa uchunguzi. 
Kwa Habari Zaidi  BOFYA HAPA  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages