Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akizungumza na mabalozi wa nchi mbalimbali kuhusu msimamo wa Tanzania katika migogoro ya nchi za Ivory Coast, Madagascar, Sudan, Somalia pamoja na vurugu zilizojitokeza mkoani Arusha wakati wa maandamo ya wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na jeshi la polisi. (Kulia) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Sazi Salula (kushoto) Naibu Waziri Mh. Mahadh Juma Maalim. WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Jeshi la Polisi lilikiuka maadili ya kazi yao, lilipokuwa likikabiliana na raia waliokuwa wakiandamana kupinga suala la uteuzi wa meya wa Arusha.
Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na vurugu zilizozuka baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa Chadema waliokuwa wanaandamana jijini Arusha wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa kwa risasi za moto.
“Jeshi la Polisi linatakiwa kufanya kazi kwa mipaka ili kuhakikisha kuwa linadumisha amani nchini,” alisema Membe akielezea kuwa ni maoni yake binafsi kuhusiana na tukio hilo linaloelekea kuliwekea doa Tanzania ambayo inajulikana kuwa ni kisiwa cha amani.
Vurugu hizo zilitokana na Chadema kuamua kuandamana kwa amani licha ya kuwepo na amri ya polisi iliyokuwa inawazuia wakishinikiza uchaguzi wa Meya wa jiji la Arusha urudiwe kwa sababu kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu zilizomsimika Gaudence Lyimo wa CCM kwenye madaraka hayo
Kwa Habari Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)