KWANINI UKUBALI KUCHANGIA PENZI? - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KWANINI UKUBALI KUCHANGIA PENZI?

 Katika PitaPita Zangu Kwenye Tovuti Nyingi Za Masuala Tofauti Tofauti Nikakutana Na Kitu Hiki Ambacho Uchukua Karibu Asilimia Zaidi ya 80 Ya Maisha Yetu Nikaona Ni kheri Niiweke Hewani Ili Wengi Waweze Kuisoma Na Kutafakari Kwa Maana Ni Kweli Ukichangia Penzi Unaweza Kujikuta Unafanya Kitu Usichokitarajia..Soma Hapa Chini........


Kati ya vitu vinavyowaumiza wengi walio katika uhusiano ni pamoja na penzi la kuchangia! Yaani uwe na mpenzi wako, halafu awe na mtu mwingine tena zaidi yako. Hakika inauma sana. Uhusiano wenye ladha ni ule wa mwenzi mmoja. Uwe wake peke yako, awe wako peke yake!


Mapenzi ni sawa na bustani nzuri ya maua, wakati mwingine inahitaji mbolea, kumwagiliwa maji na hata kupaliliwa. Kwa kufanya hivyo utazidisha ladha ya mapenzi na kuyafanya yazidi kuwa na nguvu zaidi ya awali. Lakini kama hutamwagilia, hutaweka mbolea, hutapalilia, hesabu kwamba mapenzi yako yanaweza kuanza kupoteza nguvu taratibu na hatimaye kufa kabisa.

Kikubwa ambacho nimepanga kuzungumza nanyi leo ni jinsi ya kumfanya mpenzi wako awe wako peke yako. Umeshawahi kufikiria kwamba, kama ukishindwa kutimiza mambo fulani katika penzi au ndoa yako, mwenzi wako anaweza kuwa wa kushea?

Kama bado, inakubidi ufahamu hilo kuanzia leo. Mpenzi anahitaji mambo mengi ili aendelee kuwa mwaminifu kwenye penzi lenu. Ni kweli kwamba uaminifu upo kwa mtu mwenyewe, kama mtu ni mwaminifu basi atadumisha uaminifu uliopo ndani yake, lakini kama kuna mambo unakosea, lazima utasalitiwa!

Tena basi, kama mwenzi wako anakupenda, atakusaliti huku analia! Kwanini? Kwasababu analizwa na kitendo ambacho hajapenda kukifanya ila wewe mwenyewe ndiyo umemlazimisha afanye hivyo.

Wanatafuta nini kwa wengine?
Tukiachana na tamaa, hulka na ushawishi, wakati mwingine mpenzi anaweza kusaliti kwa kukosa yale ya muhimu zaidi katika penzi au ndoa yake.

Kwa bahati mbaya sana, watu wa aina hii huwa hawasemi moja kwa moja kuwa wanakosa vitu fulani au wanapenda vitu fulani, badala yake hutumia lugha za ishara zaidi na kama hutaelewa basi huona suluhisho na kutafuta pumziko lingine nje.

Hapa sasa mwenzi wako anakuwa si wako peke yako tena! Lakini lazima uhakikishe mpenzi wako anaendelea kuwa wako bila kushea na mtu yeyote na jambo hili linawezekana kabisa ikiwa wewe mwenyewe utataka iwe hivyo.

Zipo hatua au mambo mengi ya kumfanyia mpenzi wako ili awe wako peke yako, lakini hapa nitakupa yale ya msingi zaidi yatakayokusaidia katika penzi lako.

Kama inavyoonekana hapo juu, nimeyafananisha mapenzi na bustani nzuri ambayo ina mahitaji yake. Sasa katika uchambuzi huu, nitaainisha jinsi ya kuitunza bustani (penzi) yako vizuri sana na kuifanya bora zaidi kila siku.

MOSI: Mapenzi yanahitaji mbolea. Hapa nazungumzia penzi ambalo tayari limeshakuwa penzi! Kama ni bustani basi tayari mboga-mboga zako zimemea vizuri.

Lakini ukumbuke kwamba, bustani yako haitaweza kuendelea kuwa bora kama haitakuwa na matunzo. Hapa penzi linahitaji mbolea. Mbolea ninayoizungumzia hapa ni maneno matamu yaliyojaa huba. Fikisha hisia zako kwa mwenzi wako kwa namna ya kipekee iliyojaa penzi la dhati.

Mweleze jinsi unavyompenda na jinsi maisha yako ambavyo hayawezi kukamilika bila yeye. Huu ni wakati wako wa kumsumbua kwa meseji zilizojaa tungo za mahaba, kadi, maua na zawadi ndogo ndogo.

Baadhi ya wanandoa wakishaoana, huacha utaratibu huu. Kuna wanaosema: “Ah! Hayo mambo ya kizamani bwana, kipindi akiwa demu wangu, sasa hivi yupo ndani, kwanini nihangaike?”
Haya ni makosa makubwa ndugu yangu. Shamba bila mbolea kuna mavuno kweli?

PILI: Bustani yako itahitaji maji kwa ajili ya kuzidisha ustawi wa mazao yako. Hapa unatakiwa kuwa mbunifu zaidi katika mambo yanayohusu mapenzi moja kwa moja.

Unatakiwa kubadilisha mitindo ya chumbani, mahali pa kukutana na hata sehemu za mitoko. Inashauriwa ili kuboresha penzi ni vizuri kutoka sehemu mbalimbali na mwenzi wako. Inapendeza zaidi angalau mara tatu kwa miezi sita, kulala na mwenzako hotelini.

Hapa utakuwa unanakshi zaidi penzi lako. ‘Outing’ yako ni vyema ikawa ya kimahaba zaidi, kuanzia mavazi, sehemu mnazotembelea n.k

Mfanyie mwenzi wako mambo ya kimahaba mnapokuwa wawili. Mbusu, mkumbatie, mwambie jinsi unavyojisikia wa pekee kuwa wake.

TATU: Baada ya muda bustani huota majani mengine ambayo si mboga! Yawezekana kabisa, kwa bahati mbaya uchafu ukaingia bustanini. Wakati wa palizi ni muda sahihi wa kuondoa vyote hivyo.
Hata katika mapenzi pia hutakiwa kufanya jambo hili. Kugombana au kupishana kiswahili kwa wapenzi ni jambo la kawaida sana, hivyo ni vyema kuweka sawa tofauti hizo mapema, kabla tatizo halijawa kubwa zaidi. Hii ndiyo palizi ninayoizungumzia.

Usikae na kinyongo moyoni mwako, kuwa mjanja, hata kama ni yeye ndiye aliyekosea, zungumza naye ukimweleza jinsi ambavyo hupendi mgombane, mkimweleza hisia zako kwamba unatamani sana muelewane katika siku zote za maisha yenu. Weka mambo sawa.

Kwa kufanya hivi, kwa hakika penzi lako litazidi kuwa imara zaidi na atakuwa wako peke yako. Hatakuwa wa kuchangia tena. Naamini umeibuka na kitu kipya leo.

1 comment:

  1. Kamby Shabani3:51 PM

    yes this is really happening and 2 b honesty it pains more than the pain itself,
    if u love your partner please play safe be with one only!

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages