Wanafunzi Wa UDOM Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Na Lugha Walipokua Wakimsubiri Mtoto Wa Mkulima Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda Alipokua Ndani Ya Block 3 wakati anakagua na Kujionea Miundombinu Mibovu.
Wanafunzi Wa UDOM kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Na Lugha Walipokua Wakimkimbilia Mtoto Wa Mkulima Mh.Pinda Mchana Huu Wakati Anaenda Kukagua Na Kujionea Miundombinu Mibovu iliyopo Block 5 ambalo Linakaliwa Na Wanafunzi Wa Kike Chuo hapa
Wanafunzi Wa Kitivo cha sayansi Ya Jamii Na Lugha WalipoKua Wakimshangilia Na kumfuata Popote Alipokua Akienda Mtoto Wa Mkulima Kama Wanafunzi Wengi Walivyokua Wakimuita Mh Pinda Mchana Huu
Waziri Mkuu Mh Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mtoto Wa Mkulima) kama wengi wanavyomjua Alipokua Akitazama Mazingira Machafu Yaliyopo Kwenye Makazi Ya Wanafunzi Wa UDOM kitivo cha sayansi Ya Jamii Na Lugha Muda Huu Mchana.
Wanafunzi Wakiwa Pamoja Na Mtoto Wa Mkulima Mh Pinda Wakati Akiangalia Uchafu Uliopo Kwenye Mazingira Ya Kitivo Hicho Muda Huu Mchana.Kabla Hajaelekea Kitivo Cha Elimu
Mtoto Wa Mkulima Mh Pinda Anapewa Maelekezo Ya Kutosha Na Baadhi Ya Watendaji Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Kwanini Mazingira Ni Machafu.
Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Na Lugha wakimsahangili Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda Wakati akitoka Block 5 kukagua Maeneo Ya Chuo Mchana Huu.Wanafunzi Wakisikika Wakimuita Mtoto Wa Mkulima huku Wakimshangilia Na Kupigia Makofi.Baadhi Ya wanafunzi Walisikika Wakiimba "Hatumtaki Mlacha hatumtaki Mlacha"
Mtoto Wa Mkulima Mh Pinda Alipokua Akitoka Kukagua Makazi ya Wanafunzi Wanaoishi Block 5.Mh Pinda Ajionea Hali Ya Uchafu Uliopo Kwenye Makazi Ya Wanafunzi Hao Mchana Huu Udom.Kulia kwake ni Mkuu Wa Shule Ya Lugha Prof Bagumiya.
Waziri Mkuu Mh Pinda Alipokua Akiwapungia Mikono Wanafunzi Wa Kitivo cha sayansi Ya Jamii Na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma huku akiingia ndani ya Gari lake tayari Kuelekea Kitivo Cha Elimu Muda mfupi baada ya Kukagua Na Kujionea Miundombinu Mibovu Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Mchana Huu Kabla Hajaelekea Katika Kitivo cha Elimu.
Wanafunzi Wa Udom Wakimshangilia Mtoto wa mkulima Mh Pinda Wakati wa Msafara Wake ulipokua Ukiondoka Kuelekea Kitivo cha Elimu Cha Chuo Kikuu cha Dodoma Mchana Huu. Wakati Huo Huo Wanafunzi Hao Walikuwa Wanamzomea Makamu Mkuu Wa Chuo Utawala,Fedha na Mipango Profesa Shabani Mlacha Wakati Wengine Wakizuia na Kumzomea Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Dkt Msekela Mchana Huu.Kuwasili Kwa Waziri Mkuu Pinda Kumeonyesha Jinsi Gani Wanafunzi Walivyokuwa na Imani Kwamba Ana uwezo wa kutatua Matatizo Yanayowakabili Wanafunzi Pamoja Na Wahadhiri Ambao Wamegoma kufundisha Takribani Wiki Moja sasa.Waziri Mkuu Pinda Amefika Chuo Hapa Baada ya Wahadhiri Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Kugoma Kufundisha Mpaka pale Watakapotimiziwa Mahitaji Yao pamoja na hayo waziri Mkuu Amekuja Chuo Hapa Kutatua Matatizo ya Wanafunzi Wa Kitivo Cha Elimu Na Kuangalia Hali Ya Mazingira Ya Chuo Hiki Cha Dodoma.Picha Zaidi zitawajia Muda Si Mrefu.
Picha Na Habari Kutoka Kwa Mdau Wenu LUKAZA JOSEPHAT
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)