Kwa jina halisi anaitwa John VN Shariza lakini kwa jina la kisanii anatambulika kama Man Water,ambaye ndiye mmiliki wa studio Combination Sounds'Combinega',kama vile haitoshi ndiye producer wa msanii Twenty Percent (20%) ambaye anatamba na nyimbo zake mbili kama vile 'Yanini Malumbano' na 'Tamaa Mbaya',ambazo zote zinafanya vizuri sana ktk vituo mbalimbali vya redio hapa Bongo na kwingineko
Kufuatia kazi nzuri aifanyayo msanii wake,Producer Man water mapema jana mchana aliamua kumsuprise msanii wake 20% kwa kumpeleka kwenye duka moja la vyombo vya muziki lililoko maeneo ya Kariakoo na kununulia vifaa kadhaa likiwemo gitaa.
"Nimemkabidhi zawadi hii ikiwa ni hatua ya kwanza na haikuwahi kutokea kwa maproducer wa hapa bongo,kuonyesha kukubali kazi ya wasanii wao,mpaka kutoa zawadi...mimi nimeweka historia kwakua wa kwanza kufanya hivi na pia kuzidi kumpa support ya kusonga mbele ktk muziki wake ndani na nje ya nchi" alisema producer huyo ambaye studio zake ziko maeneo ya kinondoni karibu na bar ya zamani iliyoitwa Shentembaa.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)