Meneja Mkuu wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa kutangaza siku ya fainali za mashindano ya BONGO STAR SEARCH uliofanyika mchana huu Savannah Lounge,Benjamin Mkapa Tower.kushoto ni Mkurugenzi wa Benchmark Productions,Madam Ritha Paulsen akifuatilia mkutano huo.Fainali hizo zimepangwa kufanyika Desemba 17,2010 katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil. 30 kwa ajili ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya hayo ya Bongo Star Seatch 2010 kwa Mkurugenzi wa Benchmark Productions,Madam Ritha Paulsen.katikati ni Mratibu wa BASATA,Bi. Vicky Temu.
Tano Bora wa Bongo Star Search 2010 wakiwa wameshikilia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil. 30 atakayoipata mshindi wa mashindano hayo.wengine ni Mkurugenzi wa Benchmark Productions,Madam Ritha Paulsen (tatu kushoto),Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo,George kavishe (katikati) na kulia ni Mratibu wa BASATA,Vicky Temu




No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)