wadau wa UWF
Meza ya wadau
Meza kuu pamoja na wanachama wa UWF na waume zao. Walioketi kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngereja, akifuatiwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu na mgeni rasmi Mama Margaret Chacha
Mmoja wa washindi wa bahati nasibu akipokea zawadi yake |
Mmoja wa washindi wa bahati nasibu akipokea zawadi yake |
Tovuti ya UWF ilipozinduliwa |
Baadhi ya wadau waliohudhuria |
Baadhi ya wadau waliohudhuria
Meza ya TOTAL Tanzania limited ilisheheni mameneja |
Mshindi wa zawadi ya blender toka Mini Argos akifurahia zawadi yake baada ya kushinda bahati nasibu.
Mama Margaret Chacha akichagua washindi wa bahati nasibu ya UWF
Mshindi wa zawadi ya blender toka Mini Argos akifurahia zawadi yake baada ya kushinda bahati nasibu.
THT band ilikuwepo kutumbuiza
Mwenye gauni la buluu ndiye aliyenunua mchoro wa picha ya mtoto wa kimasai kwa dola 1,500
Wana UWF wakifurahia kusikia kwamba milioni 47 zimepatikana katika hafla hiyo.
----------------
Jumla ya shilingi milioni 47 zimepatikana katika hafla ya kuchangia mfuko wa kusomesha mtoto wa kike (SOMKI) iliyoandaliwa na Unity of Women Friends (UWF), ambao ni umoja wa kinamama 11 ambao unajishughulisha na kusaidia wasichana katika masomo.
Wanachama wa UWF, ambao ni kinamama wanaofanya kazi maofisini huku wengine wakiwa ni wajasiriamali, pia walisherehekea miaka mitano ya umoja wao katika hafla iliyoafana sana katika ukumbi wa Kibo wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam Ijumaa usiku.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkurugenzi mkuu Mama Margaret Chacha, ambaye aliahidi UWF kwamba benki yake itatoa kila aina ya msaada katika kufanikisha azma yao ya kusomesha mtoto wa kike.
Watu mashuhuri wengine waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu, Mbunge wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha wa zamani Mama Zakhia Meghji, pamoja na watu mashuhuri kadhaa.
Mama Chacha pia alikata keki na kuzindua tovuti ya UWF yenye lengo la kutangaza shughuli za umoja huo ambao umekuwa mfano wa kuigwa kwa kinamama wenye moyo wa uzalendo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)