Rais Jakaya Kikwete akiwa katika gari maalum na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange wakati akiwasili ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar leo.
Amir Jeshi Mkuu,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride jana katika maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru ndani ya Uwanja Uhuru,Jijini Dar es Salaam Jana.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwasili katika jukwaa kuu.wengine ni Rais wa Zanzibar,Dr. Ali Mohamed Shein (wapili kulia) na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (wapili kushoto).
Baadhi ya Askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima kwa Amiri Jeshi mkuu.
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
RAIS Jakaya Kikwete leo aliuongoza umati wa Watanzania katika sherehe za miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambapo alikuwa ni miongoni mwa watu walioshangiliwa katika sherehe hizo.
Ushangiliaji huo, ulionekana wakati Rais Kikwete alipoingia katika Uwanja wa Uhuru , alipokuwa akisalimia wananchi akiwa anazunguka uwajani hapo.
Sherehe hizo zilipambwa na mbwebwe ya watu mbalimbali walioonekana wakiwa na furaha na kushangilia viongozi waliokuwa wakiwasili katika uwanja huo.Miongoni mwa viongozi walioshangiliwa ni Rais Mstaafu Serikali ya Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alishangiliwa na watu huku wakisema “mtoto wa mkulima’ , Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)