WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja
-------
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema tatizo sio kujiuzulu, bali ni jinsi ya kutatua kero za umeme na kuhakikisha mgawo wa umeme unakwisha nchini.
Ngeleja alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na madai ya kutakiwa kufanya hivyo kama ambavyo Mbunge wa Jimbo la
Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila alivyodai kupeleka hoja binafsi bungeni ya kutokuwa na imani naye.
Ngeleja alisema hayo ni mawazo ya Mbunge huyo na kamwe hawezi kuzuia mtu kutoa maoni yake kwa kuwa ana hisia kali kama ambavyo yeye (Ngeleja) anazo.
Madai ya Kafulila aliyatoa wakati alipotangaza kuwa anakusudia kupeleka hoja binafsi katika Mkutano wa Pili wa Bunge, Februari mwakani kutaka serikali iwajibike kwa kuliingizia Taifa hasara kwenye sekta ya umeme, kutokana na hukumu ya kesi ya Dowans na Tanesco ambayo Tanesco inapaswa kulipa Sh bilioni 185.
Kafulila pia anakusudia katika hoja hiyo, kulitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini, kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati na Mpango Kabambe wa Usambazaji wa Umeme nchini.
“Tatizo sio kujiuzulu, bali tatizo ni kufuatilia na kutatua kero za umeme zinazowasumbua wananchi.kwa habari zaidi bofya na Endelea....>>>>>>>

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)