Dkt Msekela Akisalimiana Na Principal Wa Chuo Cha Sanaa Na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha DODOMA hapo Jana Prof Bagumiya
...........................................
Mkuu wa Mkoa Wa DODOMA Dkt Msekela akiwasili Kwenye Mkutano Uliofanyika Jana Asubuhi Katika Makazi Ya wanafunzi Wa UDOM katika Kutatua Matatizo Yaliyopelekea MGOMO
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idrisa Kikula Akimkaribisha Waziri wa Mambo Ya Ndani Na Mwenyikiti Wa Bodi Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Mh Shamsi Vuai Nahodha Kuongea Na Wanafunzi
Waziri Wa Mambo Ya Ndani Na Mwenyekiti Wa Bodi Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Mh Shamsi Vuai Nahodha Akitoa Maelezo Juu Ya Ufumbuzi Wa Matatizo Yaliyosababisha Mgomo
Waziri wa Elimu Mh Shukuru Kawambwa Akitoa Maagizo Ya Kina Juu Ya Matatizo Yaliyosababisha Mgomo Tatizo Kubwa Lilikua Ni Mafunzo Kwa Vitendo Ambalo Lilikua Kero tangu Chuo Kuanzishwa Katika Baadhi ya Kozi Kulikua Hakuna Mafunzo Kwa Vitendo yaani Field. Waziri Wa Elimu Aliagiza Uongozi Wa Chuo Kuhakikisha Kozi zote ambazo Hazina Mafunzo Kwa Vitendo Ziw Nazo Na Prospectus ibadilishwe haraka Sana
Wanafunzi wa UDOM walipokuwa wakiwasikiliza Mawaziri na Raisi Wa Chuo Cha Sayansi Ya Jamii Na Lugha Kwa Makini
Wanafunzi Wa Udom Chuo Cha Sayansi Ya Jamii Na Lugha Wakishangilia Mara Baada Ya Waziri Wa Elimu Kutoa Agizo Na Kuamuru Kuwa Mafunzo Kwa Vitendo Kwa Kozi Zilizokosa Sasa Kuwa Na Mafunzo Kwa Vitendo.
Hilo Ni Bango Mojawapo Ambalo Linalaani Nguvu Ya Polisi Iliyotumiwa Na Polisi Katika Maandamano Ya Amani Ambapo Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Dkt Msekela Aliamuru Polisi Kutumia Nguvu Na hatimaye Polisi Kutumia Mabomu Ya Machozi.
Bango Ambalo lilikua likilaani Nguvu Ya Polisi Iliyotumika Likiwa Limewekwa Juu Ya Gari La Principal Wa Shule Ya Sayansi Ya Jamii Prof Mwamfupe mara baada ya mkutano kumalizika.Wakati huo huo Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Wakati Akiondoka Wanafunzi Walimzomea Mkuu Huyo Wa Mkoa Kwa Kile ambacho aliruhusu Polisi kutumia nguvu na hatimaye kujeruhiwa na kuharibu mali za wanafunzi na chuo kutokana na mabomu ya machozi.
Habari Na Picha Kutoka Kwa RIPOTA WAKO JOSEPHAT LUKAZA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)