Leon Bahati
HATIMAYE dunia sasa inaweza kuwa na matumaini ya kuondokana na ugonjwa hatari wa Ukimwi baada ya chanjo ambayo iligunduliwa mwezi Julai mwaka huu na wanasayansi wa Marekani, kuanza kufanyiwa majaribio.Wagunduzi wa kinga hiyo walitamba mwezi Julai kuwa chanjo hiyo ina uwezo wa kukabiliana na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa asilimia 90, na sasa wanahamasisha watu ambao hawajaambukizwa Ukimwi kujitokeza katika majaribio ya chanjo hiyo.
Hatua ya kufanyiwa majaribio kwa kinga hiyo imekuja baada ya wagunduzi hao ambao ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaid) ya nchini Marekani kufanikiwa kuhamisha teknolojia ya dawa hiyo kutoka kwenye maabara.
Kwa mujibu wa taarifa ya Niaid iliyotumwa kwa Mwananchi wiki iliyopita, majaribio ya chanjo hiyo yatawajumuisha maelfu ya watu duniani kote na wengi wanahamasishwa kujitokeza ili kufanikisha utekelezaji wa hatua hiyo.
Mkurugenzi wa Niaid, Profesa Anthony Fauci anaeleza kwenye taarifa hiyo kwamba anatarajia majaribio hayo yanaiingiza dunia katika zama mpya za kuvikabili virusi vya ukimwi.
Mkurugenzi huyo pia anawataka watu kujitokeza kwa wingi kujitolea kufanyiwa majaribio, kwa kuwa hatua hiyo itaifungulia njia taasisi yake kupata kibali cha Shirika la Afya Duniani (WHO) cha kuanza kutumika kwa dawa hiyo duniani kote.

Kwa Taarifa Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)