BENKI KUU YA TANZANIA KUZINDUA NOTI MPYA IJUMAA HII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BENKI KUU YA TANZANIA KUZINDUA NOTI MPYA IJUMAA HII

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Benno Ndulu
----
 Ijumaa wiki hii Benki Kuu Tanzania itazindua noti mpya katika shughuli itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki hiyo.Noti hizo mpya zitazinduliwa wakati wataalamju wa uchumi wamekuwa wakisema ni vyema uchakavu wa shilingi ukaangaliwa upya.

Kuanzia mwaka 1966 kumekuwa na mabadiliko kadhaa katika fedha ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kupanda kwa dinominesheni husika.Mathalani mwaka 1966 kulikuwa na noti ya shilingi 20 iliyokuwa na sura ya Nyerere na shilingi 100 iliyokuwa na mmasai pamoja na nyingine iliyokuwa na simba.
Na Mwaka 1978 zilitolewa noti za shilingi 10 na shilingi 20.

Mabadiliko mengine katika sura ya noti yalifanyika pia miaka ya 1985, 1987, 1989,1990kwa kuwa na noti ya shilingi 50 ambamo alikuwamo Mwinyi na punda milia na masuala ya mavuno.Noti ya shilingi 1000 yenye sura ya mwinyi na tembo iliingia mwaka 1993 na mwaka 1995ilingia noti ya mwinyi na simba ya shilingi 10000 .

Mwaka 2000 kuliingizwa noti ya shilingi 1000 ikiwa na sura ya Nyerere, tembo na mgodi wa makaa ya mawe, mwaka 2003 kukaingizwa noti ya shilingi 500 ikiwa na nyati na hospitali na mwaka 2003 iliingia noti ya shiling200 ikiwa na mji Mkongwe na mlima Kilimanjaro.Pia mwaka huo huo iliingia noti ya shilingi 5000 ikiwa na faru na mgodi na noti ya shilingi 10000 ikiwa na jengo la benki na tembo.

Kuna matoleo mengi ambayo siku yaandika hapa, lakini mara nyingi mabadilkiko ya matoleo hutokana na kuhifadhi historia na pia kujaribu kurekebisha mzunguko wa fedha na thamani yake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages